KENYA: SIMBA WAWILI WAONEKANA BARABARANI NAIROBI
                      Posted in 
                      
afrika mashariki
                            No comments
                          
Monday, February 29, 2016
                      By 
                      danielmjema.blogspot.com
Simba wawili wameonekana katika 
barabara moja ya mji mkuu wa Kenya, Nairobi wiki moja tu baada ya simba 
wengine kutoroka kutoka mbuga ya taifa ya Nairobi.
Simba hao walionekana na polisi wa trafiki, waliokuwa wakipiga doria katika barabara ya Southern Bypass, mwendo wa saa nne asubuhi, shirika la huduma kwa wanyamapori (KWS) limesema kupitia taarifa.
Wanyama hao walionekana wakitembea karibu na ua unaozunguka msitu wa barabara ya Ngong, karibu na kituo cha idara ya misitu ya Kenya (KFS).
Polisi hao waliwapasha habari maafisa wa KWS ambao wameanza operesheni ya kuwatafuta wanyama hao.
Siku kumi zilizopita, simba sita waliotoroka kutoka mbuga ya taifa ya Nairobi walionekana katika eneo lenye watu wengi la Langata.
Baadaye, simba jike na shibli wake walipatikana na wakarejeshwa kwenye mbuga hiyo. Simba hao wengine inaaminika walirejea wenyewe kwenye mbuga.
CHANZO: BBC SWAHILI
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako


0 MAOINI :