TANZANIA: WADAU WAAANZA KUJENGA UELEWA KUHUSU SIKU YA MAGONJWA YANAYOTOKEA KWA KUNDI DOGO LA JAMII
Posted in
afrika mashariki
No comments
Monday, February 29, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Wadau hao wakinyoosha mikono juu kuonesha umuhimu wa kuadhimishwa kwa siku hiyo ya Magonjwa Yanayotokea kwa kundi dogo la jamii ndani ya jamii.
Mratibu
wa tukio hilo Bibi Sharifa Mbaraka akizungumza mbele ya Waandishi wa
habari (hawapo pichani) kwenye moja ya ukumbi wa hoteli ya Serena leo
jijini Dar,Bi.Sharifa alisema kuwa tukio hilo limedhamiria
kujumuisha vyombo vya habari na wadau wengine ili kujenga uelewa kuhusu
magonjwa hayo.
“Yapo
magonjwa tofauti yanayowasibu watu wachache takribani 7000 ambayo
yameshabainishwa duniani hadi leo na Tanzania haiwezi kujitoa
kwenye hili. Hata hivyo watu wengi hapa Tanzania hawana uelewa kuhusu
magonjwa hayo”,alisema Bi Sharifa ambaye watoto wake wawili Ali Mohammed
Kimara 5, na Nasreem Mohammed 3, wanasumbuliwa na magonjwa hayo.
Alifafanua
kuwa kutokana na uzoefu wake, amepata msukumo na kuamua kuwaunganisha
wazazi, wagonjwa walio na magonjwa hayo na raia wenye mapenzi mema ili
kujenga uelewa muhimu na kutoa wito kwa jamii kuchukua hatua.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :