INASIKITISHA: Mtunisi afikishwa mahakamani kwa kumpiga mkew

Posted in
No comments
Wednesday, December 3, 2014 By danielmjema.blogspot.com


Mtunisi alipandishwa katika Mahakama ya Mwanzo Manzese Sinza jijini Dar es Salaam Jumatatu iliyopita, ambapo baada ya kusomewa shtaka lake la kushambulia mwili, mtuhumiwa alikana na hivyo hakimu kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena.

Hata hivyo, Mtunisi alishindwa kupewa dhamana baada ya hakimu kutoridhishwa na afya ya mwanamke huyo, Aziz ambaye anaugulia nyumbani.
Katika hali nyingine, walinzi wa mahakama hiyo walionyesha mizengwe mikubwa kwa waandishi wa habari hizi, kwa kuwazuia kuingia ndani ya chumba cha mahakama wala kupiga picha, kwa madai kwamba sheria zao haziruhusu.
Wakionekana kama waliopewa maelekezo maalum, waliwataka kupeleka barua kutoka chombo chao cha kazi, kwani hata baada ya kuwakumbusha kuwa zoezi hilo lilishafanyika siku za nyuma, badala ya kupekua mafaili yao ili kuiona barua hiyo, waliwataka kwenda kuleta nakala ya barua iliyoandikwa awali, zoezi ambalo lilikuwa gumu kutokana na muda.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .