Umeme Afrika: Mkutano umepangwa kukuza biashara na ushirikiano kwa sekta za umeme za Afrika mjini Washington DC Januari hii
Posted in
Matukio
No comments
Sunday, December 14, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Umeme Afrika: Mkutano Utafanyika Katika Mji wa Washington DC, Tarehe 28-30 Januari 2015, Na Ahadi Kutoka Nchi 12 za Afrika Kukuza Ushiriki wa Sekta ya Kibinafsi Katika Sekta ya Umeme ya Afrika
WASHINGTON, December 10, 2014/ -- Kwa miaka 20 iliyopita EnergyNet imepanga mikutano ya wawekezaji na baadhi ya wakuzaji wa umeme wa kuaminika na mashuhuri wanaoendesha biashara barani Afrika. Symbion Power, GE, Siemens, Copperbelt, Goldwind, Azura Power, Aldwych, Karpowership, Globeleq, Schneider Electric, ESBi, Transcorp, Chint, China State Grid, Hanergy na makampuni mengine ambayo yametoa ahadi za muda mrefu katika sekta hii na kuwekeza katika ufumbuzi endelevu. Haya ni makampuni makubwa yenye mizania imara yanayotambuliwa na baadhi ya benki kubwa.
Licha ya mvuto, ujuzi na tajiriba hii yote, mabiliano ya madola yametumiwa katika ukuzaji kwa miaka 20 iliyopita na miradi mingi haijafikisha kikomo cha kifedha. Kwa hivyo, swali moja muhimu kujiuliza ni ni njia gani ya sasa ya kufanya mambo ndiyo ya kudumu?
Wawekezaji wanaweza kuwajibikaje kwa mafanikio na kasi ya ukuzaji wa miradi ya muda mrefu inayoendelea? Hatimaye, serikali za Afrika na sekta ya umma ndio "mamlaka barani Afrika" na ni jukumu lao kujenga stesheni za umeme na kusambaza umeme kwa watu. Usambazaji wa umeme unaweza kuongeza manufaa kwa wote, lakini jambo la muhimu pia ni kwamba unaweza kuongeza ustawi ili kukuza uwekezaji wa sekta ya kibinafsi zaidi, kuongeza ajira zaidi na hata utajiri zaidi.
Jambo hili linaonekana likiwa rahisi.... Bila shaka linaonekana likiwa rahisi, lakini wakati mwekezaji mtarajiwa anashirikiana barani kote na wizara zisizo na miundombinu ya teknolojia na uzoefu wowote wa kimataifa katika idara zote, anaanza kuelewa changamoto ambazo serikali na wakuzaji wanakumbana nazo wakijaribu kukubailiana.
Mwaka uliopita tuliona mabadiliko katika mazungumzo na mabadiliko ya kuelekea upande mzuri unaolenga ujenzi wa uwezo na usaidizi wa miundombinu kwa mashirika ya sekta ya umma.
Symbion Power, Schneider, GE, Aggreko, na Norton Rose Fulbright na makampuni mengine yamekuwa yakiwekeza katika ujenzi wa uwezo wa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya kiwango cha chini.
Makampuni haya, pamoja na PwC na Deloitte yanashirikiana na mashirika ya sekta ya umma katika miradi zaidi ya ukuzaji ili kusaidia ujenzi wa uwezo. Hatua moja muhimu imekuwa kuzinduliwa kwa mpango wa "Umeme Afrika" wa Rais Obama ulioundwa kuongeza upatikanaji wa umeme katika Afrika yote Kusini mwa Sahara.
Mpango wa Umeme Afrika unataka kuimarisha uwezo wa mashirika na watu unaohitajika kuvutia uwekezaji kwa misingi endelevu ya muda mrefu na kudhibiti sekta ya umeme inayokua kwa ufanisi.
Tangu kuzinduliwa kwake mwishoni mwa Juni 2013, mpango wa Umeme Afrika umesaidia kurahisisha uhusiano wa kifedha wa miamala ya sekta ya kibinafsi ambao unatarajiwa kuzalisha zaidi ya Megawati 3,100 (MW) za uwezo wa uzalishaji mpya. Zaidi ya hayo, mpango wa Umeme Afrika tayari umegawanya zaidi ya dola bilioni 20 kama ahadi kwa zaidi ya wabia 80 wa sekta ya kibinafsi.
Mpango wa Umeme Afrika pia umeingia katika ubia wa kimkakati na Benki ya Dunia, Benki ya Ukuzaji ya Afrika na Serikali ya Uswidi, ambao kwa jumla wameahidi dola bilioni 9 zaidi.
Katika 'Mkutano wa Umeme Afrika' (http://www.poweringafrica- summit.com): utakaofanyika Washington mwezi ujao nyingi ya changamoto na fursa zitajadiliwa, wengi wa wawekezaji walio katika mpango huo wakihudhuria ikiwa ni pamoja na wale kutoka AfDB, Benki ya Dunia, Serikali ya Marekani na wabia wa sekta ya kibinfasi.
Tukiwa na ushirikiano kama huo wa nguvu kati ya wawekezaji wa kimataifa, tuna uhakika kwamba sio jambo la 'kama' utaleta fursa, bali ni 'wakati' fursa hizo zitaabadilisha maisha ya walio mashinani.
Ikiwa imelenga sekta ya umeme ya Afrika na uzalishaji wa umeme katika masoko yanayokua kwa miaka 20, EnergyNet imepata fursa ya kushuhudia juhudi na ahadi ya muda mrefu inayohitajika 'kuwasha taa barani Afrika.' Leo kuna shauku kubwa na 'matarajio' zaidi kuhusu uwezo wa soko la umeme la Afrika, na tunafurahia kushiriki katika jukumu dogo kama hilo katika sekta muhimu na ya kusisimua.
Kuanzia tarehe 28-30 Januari 2015, EnergyNet itakaribisha wajumbe wa Wizara na maofisa kutoka mashiriki ya huduma na udhibiti kutoka Afrika kwa mkutano na washikadau wa sekta ya kibinafsi na umma ya Marekani katika Mkutano wa Umeme wa Afrika: ambapo wataendelea na mazungumzo muhimu kuhusu jinsi ya kudumisha kasi ya kujenga sekta ya umeme Afrika.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :