WAKENYA WAWAFUNIKA WATANZANIA MICHUANO YA TENISI DAR OPEN

Posted in
No comments
Sunday, December 14, 2014 By danielmjema.blogspot.com

DSC_0453
Mmoja wa wadhamini kutoka kampuni ya mawikili ya IMMA ya Dar es Salaam, Alexander Sarac, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa michuano ya tenisi ya walemavu ya kimataifa kutoka Tanzania kwa udhamini mkuu wa kampuni ya magari ya CFAO Motors kupitia brandi ya magari ya Mercedes Benz. (Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu
WACHEZA tenisi kutoka nchini Kenya wamewafunika watanzania katika michuano ya kimataifa ya kwanza ya tenisi kwa walemavu (Dar Open ).
Michuano hiyo inatarajiwa kuhitimishwa kesho katika viwanja vya Gymkhana, majira ya saa 10 ambapo washindi watapewa tuzo zao.
Kwa mujibu wa matokeo ya hadi mchana wakati mwandishi wa habari hizi anaondoka viwanjani hapo, mechi saba zilienda kwa wakenya kwa nafasi ya wanaume na wanawake na mbili ndio walishinda Watanzania.
Michuano hiyo ambayo inadhaminiwa na kampuni ya magari ya CFAO, Mercedes-Benz na kampuni ya mawakili ya Dar es salaam ya IMMMA imelenga pia kuandaa wachezaji kwa ajili ya mechi za kufuzu michezo ya dunia zinazotarajiwa kupigwa nchini Kenya Februari mwakani.
DSC_0413
Mshiriki wa michuano ya tenisi ya walemavu ya kimataifa kutoka Tanzania, Rehema Selemani akirusha mpira wakati akichuana na mshiriki kutoka Mombasa, Phoebe Masika (hayupo pichani).
Kwa mujibu wa msemaji wa wadhamini wa michuano hiyo Alexander Sarac, michuano hiyo yenye washiriki wanaume 17 na wanawake watano walioitwa kutoka Tanzania na Kenya, imelenga kuwezesha walemavu kuendeleza vipaji vyao vya kucheza tenisi.
Pamoja na kuwa na ushindi dhaifu wa watanzania kocha wa timu ya Tanzania amesema bado ana bunduki zake mbili na ana hakika kesho vikombe vitabaki Tanzania.
Fungua dimba ya michuano hiyo ilianzishwa na watanzania Novatus Temba na Moses Sebastian ambapo Temba alimchapa Sebastian kwa seti 2-0; mkenya Itaken Timoi alimvuruga Bernad Antony kwa seti 2-0 huku Mkenya mwingine Peter Mnuve akimtoa Mtanzania Albert John kwa seti 2-0.
DSC_0376
Katika michezo mingine Rajab Abdallah kutoka Kenya alimtoa Adil Hashim kwa seti 2-0 huku Yohana mwila wa Tanzania akimpa taabu Kenya ambaye alimuondoa kwa seti 2-1.
Muingereza anayeishi nchini Ian Artetiel alimtoa Mtanzania Voster Peter kwa seti 2-1.
Mkenya Caleb Odisyo alimchapa Mtanzania Wiston Sango kwa seti 2-0 wakati katika mechi za wanawake, Mtanzania Rehema Seleman alimsulubu bila huruma Asia Mohamed wa Kenya seti 2-0.Katika mechi nyingine Asia Mohamed alimchapa Bihawa Mustafa kwa seti 2-1.
Naye Lucy Shirima wa Tanzania alitandikwa na Phoebe Masika wa Kenya kwa seti 2-0.
Timu ya Tanzania ambayo kwa sasa ndiyo inayotamba Afrika Mashariki kutokana na michuano ya mwisho iliyofanyika Nairobiu kutwaa ushindi ina kazi ya ziada kulinda heshima yake.
DSC_0404
Mshiriki kutoka Mombasa, Phoebe Masika akishiriki mashindano hayo.
DSC_0418
Mtinange ukiendelea.
DSC_0499
Mshiriki wa michuano ya tenisi ya walemavu ya kimataifa kutoka Tanzania Yohana Mwila (kushoto) akipeana mkono na mshiriki mwenzake kutoka Mombasa, Rajabu Abdallah mara baada ya kumaliza mchezo wa seti 3 ambapo seti ya kwanza Rajabu Abdallah ameshinda 4-3 na seti ya pili ameshinda Yohana Mwila 4-3 na ya tatu ubingwa ukienda kwa Yohana Mwila 10-3 katika kutafuta mshindi wa robo fainali kwenye michuano hiyo iliyodhaminiwa na kampuni ya magari ya CFAO Motors, kupita brandi ya Mercedes-Benz kama wadhamani wakuu na kampuni ya mawakili ya Dar es salaam ya IMMMA.
DSC_0421
Ofisa wa Kitengo cha masoko na huduma wa CFAO Motors Ltd, Angel Ndege akiwa amejumuika na washiriki hao uwanjani hapo.
DSC_0423
Baadhi ya washiriki kutoka Tanzania na Mombasa wakishuhudia wenzao wakiumana uwanjani.
DSC_0436
Vikombe vitakavyokabidhiwa hapo kesho kwenye fainali za michuano hiyo.
DSC_0488
Ofisa wa Kitengo cha masoko na huduma wa CFAO Motors Ltd, Angel Ndege na Kocha wa timu ya wachezaji tenesi Tanzania, Riziki Salum wakiangalia vikombe vitakavyokabidhiwa kwenye fainali za michuano hiyo itakayorindima hapo kesho kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
DSC_0433
Mmoja wa wadhamini kutoka kampuni ya mawikili ya IMMA ya Dar es Salaam, Alexander Sarac (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wadau wa mchezo wa tenesi waliofika uwanja hapo kushuhudia michuano hiyo.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .