Yote Uliyowahi Kutaka Kujua Kuhusu Mkito.com: Mahojiano ya Bongo Celebrity na Mwanzilishi Mwenza,Sune Mushendwa
Posted in
Burudani
No comments
Tuesday, January 6, 2015
By
danielmjema.blogspot.com
Sune Mushendwa
Kwa miaka nenda rudi, wasanii wa kitanzania walikuwa na kilio kinachofanana. Ungekaa pembeni bila kuwaona, ungedhani kutokana na mwangwi wa kilio chao, anayelia ni mmoja. Hapana. Wote walikuwa [na pengine bado wanaendelea kulia] kutokana na kunyonywa “jasho lao”. Kimsingi “jasho” wanalolilia limekuwa ni soko na usambazaji. Kipaji unacho na watu wanakubali kazi zako.
Tatizo utaifikishaje kazi yako kwa mashabiki zako? Ni wazi kwamba unahitaji msaada wa kimasoko na usambazaji. Kusema utaweza kufanya kila kitu peke yako ni kujidanganya.Nani? Yupo wapi na utampa kazi zako kwa thamani gani? Kilio chao kilianzia hapo.
Wengine wakaamua kuachana na muziki [wengine muziki umewaacha wao] kutokana na ukosefu wa soko la uhakika na kuona kadhaa ya kupanga foleni ukisubiri “hela yako”.
Mabadiliko ya masoko ya kazi za wasanii duniani kutoka kwenye mifumo ya ki-analojia kwenda kwenye dijitali na pia kutoka katika mifumo ya vitu kama CD mpaka kwenda kwenye matumizi ya simu na vikabrasha vingine vya mikononi, kulimaanisha kwamba soko la wasanii wa kitanzania [na Afrika kwa upana wake] lilikuwa linazidi kufifia. Hakuna tena shabiki anayetaka kubeba furushi la CD. Inakuwaje?
Hapo ndipo baadhi ya vijana wakaona fursa kuthibitisha kwamba penye tatizo ndipo pa kukimbilia.Fursa ni kama dhahabu au almasi.Huwezi kuiokota kando ya bahari ikiwa imetupwa ufukweni na mawimbi ya bahari. Wazo la fursa likazaa Mkito.Com mahali ambapo wasanii sasa wanapumua na huku changamoto pekee ni kuwashawishi mashabiki kupakua kazi zao kutoka Mkito.Com. Kila mara shabiki anapofanya hivyo, msanii ananufaika na kupata nguvu zaidi ya kuingia tena studio kunogesha mambo.
It’s a win win situation. Sune Mushendwa [pichani juu] ni mwanzilishi-mwenza wa Mkito.Com.
Kujua mengi zaidi nilimtafuta na kupiga naye story kidogo. Ameelezea mengi. Nakukaribisha usome mahojiano yangu naye ili ujue yote ambayo umekuwa ukitaka kuyajua kuhusu Mkito.Com .Twende pamoja;
BC: Sune karibu sana ndani ya BongoCelebrity. Hii ni mara yako ya kwanza hapa na bila shaka wasomaji wangependa kupata japo kwa kifupi tu historia yako. Ulizaliwa wapi,ukakulia wapi na kusomea wapi na mambo kama hayo?
SM: Asante sana kwa kunikaribisha. Mimi nimekulia Arusha na ndipo niliposoma pia. Baada ya sekondari nilienda kusoma chuo kikuu nchini Finland ambako mama yangu ndipo anapotokea.
BC: Wajasiriamali wengi ambao nimewahi kufanya nao mahojiano huniambia kwamba waliamua kufanya wanachokifanya baada ya kukosa au kubughudhiwa na kitu fulani.Huwa kuna kisa au mkasa nyuma ya pazia. Kwa upande wa Mkito kuna kisa au mkasa wowote? Ilikuwaje mpaka ukasema Aha…Mkito ikaanza? Na hili jina lilikuja namna gani?
SM: Baada ya kutoka masomoni nilianzisha studio ya muziki Arusha.Lakini tatizo kubwa lililoonekana moja kwa moja ni kwamba wasanii pamoja na studio zinapata tabu sana katika kusambaza na kuuza kazi zao. Niliona tunahitajika njia ya kuweza kusambaza muziki kirahisi na pia kuingiza kipato kwa msanii. Baada ya research na maandalizi ya zaidi ya miaka 4 ndipo Mkito.com ilipozaliwa tarehe 30 April 2014.
BC: Mpaka sasa Mkito imefanikiwa kuwa na wasanii wangapi? Nini masharti ya msanii kujiunga au kuweka kazi zake katika Mkito?
SM: Kuna wasanii takriban 600 waliojiunga mpaka sasa na wanaongezeka kila siku. Masharti ya kujiunga ni marahisi, uwe umerekodi wimbo anghalau mmoja wenye ubora. Baada ya hapo msanii anaweza kujitengenezea akaunti yake kupitia tovutiwww.mkito.com na kupakia[upload] nyimbo zake mwenyewe. Msanii baada ya hapo anaweza kufuatilia mauzo yake mwenyewe kupitia akaunti yake aliyoitengeneza.
BC: Bado nikiwa katika swali au maswali ya wasanii. Msanii akishaingia katika mkataba au makubaliano na ninyi, bado anakuwa na haki na uhuru wa kuendelea kusambaza kazi zake katika platforms zingine kama vile iTunes,Spotify,Google Play nk?
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :