BARABARA KADHAA KUFUNGWA KUHAKIKISHA USALAMA WA WANARIADHA MBIO ZA KILIMANJARO MARATHON

Posted in
No comments
Wednesday, February 25, 2015 By danielmjema.blogspot.com



Baadhi ya barabara za manispaa ya Moshi zitafungwa ili kuhakikisha usalama wa wanariadha wataoshiriki mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathon 2015 zitakazofanyika Jumapili Machi mosi. 

Mkurugenzi wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo  amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Moshi imetoa kibali cha kufunga na takribani kilometa kumi za barabara kuu iendayo Dar zitafungwa kuanzia saa 12.15 asubuhi hadi saa 2.00 asubuhi.

Barabara ya Sokoine kutokea chuo kikuu cha ushirika na biashara, (MOCU), hadi KCMC na kona barabara ya Kibosho na kutoka barabara ya Lema hadi chuo kikuu cha ushirika, kupitia barabara ya Kilimanjaro, zitafunguwa kuanzia saa 12.30 asubuhi hadi saa 2.00 asubuhi.

Addison alisema kutakuwa na udhibiti utakaofanywa na askari wa usalama barabarani kwenye barabara ya kutoka YMCA hadi mnara wa Saa, Barabara ya Boma, mzunguko wa barabara ya Arusha,  Barabara ya Uru hadi ile ya 
chuo kikuu cha ushirika, zitafungwa kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi za 2.15 asubuhi.

“Madereva wote watakaotumia barabara hizi punde zitakapokuwa zimefunguliwa, wanaombwa kuendesha magari yao kwa uangalifu na tahadhari kubwa kwa ajili ya usalama wa wale wanariadha ambao bado watakuwa wanaendelea na 
mbio hizo”, alisema.

Makampuni ya kusafirisha na kuongoza watalii watakaokuwana makujukumu ya kuwasafirisha wateja wao kutokea Mweka,  yanashauriwa kuanza safari zao baada ya Saa 3.00 asubuhi kwa kupitia barabara za Mweka na Sokoine kwa vile wanariadha watakuwa washapita maeneo hayo.

 Waendesha magari na wale wa vyombo vingine vya moto wanashauriwa kuepuka kutumia barabara za Lema, Kilimanjaro na ile ya lango kuu la kuingilia chuo kikuu cha ushirika na biashara kadiri itakavyowezekana
ili kuepuka usumbufu.

Mabasi ya mikoani yanashauriwa kuanza safari zao za kutoka Moshi kuelekea Dar es Salaam baada ya Saa 2.00 asubuhi. Hata hivyo yale ya kutoka Moshi kuelekea Arusha yanaweza kufanya hivyo kwa kupitia barabara ile ya mzunguko wa barabara ya kwenda Arusha.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .