umeipata hii?....MTANZANIA KUJIUNGA NA KITUO CHA VIPAJI SENEGAL.

Posted in
No comments
Wednesday, February 25, 2015 By danielmjema.blogspot.com

Mtanzania, Nasry Daudi Aziz amechaguliwa kujiunga na kituo cha kukuza vipaji cha Aspire Football Dream kilichopo katika mji wa Dakar nchini Senegal.

Mradi wa Aspire nchini ulianza mchakato wa kusaka vijana mwezi Machi - Mei, 2014 ambapo vijana wengi walijitokeza na kuchaguliwa vijana 14 ambao walikwenda katika mchujo mwingine uliofanyika nchini Uganda uliowashirikisha vijana zaidi ya 50.
Kijana huyo ni miongoni mwa wachezaji 17 waliochaguliwa kati ya vijana 34 waliokuwepo nchini Senegal kwa muda wa mwezi mmoja, ambapo kulikuwa na vijana wengi kutoka nchi mbalimbali barani Afrika na Amerika ya Kusini.
Kituo cha Aspire kilichopo Dakar nchini Senegal ni miongoni mwa vituo viwili vinavyoongozwa na mtoto wa mfalme wa Qatar na timu ya Barcelona, kituo kingine kipo mjini Doha.
Nasry Daud Aziz anatarajiwa kuondoka nchini Februari 28 mwaka huu kuelekea Dakar ambapo atakuwa kwenye kituo hicho kwa mkataba wa miaka mitano.
Kutoka nchini Tanzania Nasry anakuwa ni kijana wa tatu kujiunga na kituo hicho, wengine ni Matine Taganzi na Orgenes Morrel ambaye aliitwa kwenye timu ya Taifa Stars maboresho na kocha Mart Nooj.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .