Bayport yazindua huduma ya mikopo kwa njia ya mtandao
Posted in
Matukio
No comments
Tuesday, March 10, 2015
By
danielmjema.blogspot.com
Msimamizi wa michezo ya kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Mrisho Milao kulia akipata maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya mtandao (Online) wa Bayport Financial Services, Zainabu Kalufya, katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao kwa www.kopabayport.co.tz, uzinduzi uliofanyika leo Makao Makuu ya Bayport, jijini Dar es Salaam. Picha kwa Hisani ya Bayport.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI yaKifedhaya Bayport Financial Services, yenye Makao Makuu
yake jijini Dar es Salaam, Tanzania, imezindua tovuti yake ya www.kopabayport.co.tz, itakayowezesha
wateja wake kupata mikopo ya haraka na kwa njia rahisi.
Kwa kupitia tovuti hiyo, watu mbalimbali wanaweza kupata huduma za
Bayport, sanjari na kupata mkopo ndani ya saa 24 baada ya kuidhinishwa, huku akijibiwa
ombi lake la mkopo, ndani ya masaa mawili tangu alipojisajiri kwa mara ya
kwanza.
Akizungumzia huduma hiyo mpya ya mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam leo mchana, Meneja Masoko na Mawasiliano
wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba huduma hiyo sasa itawawezesha
wateja wao kukopa mahala popote atakapokuwa, tofauti na awali.
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services kitengo cha Huduma kwa Wateja, wakiwajibika wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao onlinewww.kopabayport.co.tz, jijini Dar es Salaam leo.
Alisema kuwa lengo la uanzisha kwa tovuti hiyo ya www.kopabayport.co.tz ni kutokana
na kuweka sera ya mikakati ya kuwapatia huduma hiyo watu wengi iliwaweze kukopa
na kujikwamua kiuchumi, ikiwa ni maalum kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa
kampuni zilizoidhinishwa na Bayport.
“Bayport sasa imezidi kupiga hatua, kwa sababu mteja wetu hata
kama akiwa nyumbani kwake, kwa kupitia huduma yetu hii anaweza kujisajiri na kukopeshwa
anachokihitaji kutoka kwetu bila kupata usumbufu wa aina yoyote.
“Hayani mambo mazuri na naamini ni wakati wa wateja wetu na Watanzania
wote kuendelea kuchangamkia huduma zetu za mikopo, ukizingatia ni Bayport pekee
inayoweza kukupatia mkopo wa Chagua chochote Bayport italipia, Bima ya Elimu ya
Uwapendao, mikopo ya fedha na mingineyo muhimu,” alisema Cheyo.
Naye Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha, Mrisho Millao, alisema utaratibu wa kukopa kwa njia ya
Internet kutoka Bayport ni mzuri na utarahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa
wateja wao na Watanzania kwa ujumla.
“Nimeangalia ni mfumo mzuri na rahisi kwa mteja wa Bayport
kupata mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao huku ukiwa katika lugha mbili za Kiswahili
na Kingereza,” alisema Millao.
Kwa mujibu wa Cheyo, hiyo ni njia rahisi na ya haraka mno inayomuwezesha
kumpatia mkopo mteja wao, bila kusumbuka kwenda kwenye tawi kuanza taratibu za kujiunganisha
kwenye huduma za mikopo ya taasisi yao.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :