EU WAMPA TUZO MAMA HELEN- KIJO BISIMBA

Posted in
No comments
Thursday, March 19, 2015 By danielmjema.blogspot.com

MAMA
Umoja wa Ulaya umemtunuku Mama Helen Kijo- Bisimba (pichani) kutokana na mchango wake kwa ajili ya kutetea na kulinda haki za binadamu nchiini.

Tuzo hiyo, ilitolewa juzi na EU siku ya Jumanne wiki hii jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mwaka wa Maendeleo Ulaya 2015.

Balozi wa Umoja wa Ulaya bwana Filberto Sebregondi alitoa tuzo hizo na kusema kuwa lengo lake ni kusimamia haki kwenye masuala ya kiulimwengu ikiwemo kupambana na umasikini na kuhamasisha raia kujihusisha na maendeleo.

Wengine waliotunukiwa tuzo katika hafla hiyo pamoja na Mama Bisimba ni wanamziki
Keisha Saban, Fareed Kubanda (FID Q), na Balozi Mpungwe, pamoja na Paul Ndunguru ambae ni msanii na mchoraji.

EU imekuwa mstari wa mbele kupambana na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu hususani ukatili dhidi ya Wanawake na watoto ikiwemo vitendo vya ukeketaji, ndoa za utotoni, na mauaji ya vikongwe.

Vilevile, EU imekuwa mstari wa mbele kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na kupinga adhabu ya kifo.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .