KITABU CHA 'THE 7 HABITS OF HIGHLY EFFECTIVE PEOPLE' CHAZINDULIWA UPYA KWA LUGHA YA KISWAHILI
Posted in
JICHO PEVU LA KIJIWE
No comments
Tuesday, April 28, 2015
By
danielmjema.blogspot.com
Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege (kulia) akimwonyesha kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto) akipitia kurasa mbalimbali za kitabu hicho kabla ya uzinduzi rasmi. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege.
Mwezeshaji wa Franklin Covey, Alice Levora akichambua kwa ufupi tabia 7 zilizomo kwenye kitabu hicho kwa wageni waalikuwa (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi rasmi.
Na Mwandishi wetu
UWEKEZAJI mkubwa unatakiwa kufanywa katika eneo la raslimali watu, kama taifa hili linahitaji kuondokana na malalamiko kuhusu maendeleo na ajira.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemia Mchechu wakati akizindua tafsiri ya kiswahili ya kitabu cha “The 7 Habits of Highly effective people” kilichoandikwa na Mmarekani, Stephen Covey.
Hii inakuwa tafsiri ya kwanza ya kitabu hiki kwa lugha za asili zinazotumika bara la Afrika . Alisema malalamiko mengi kuhusiana na taifa kuwa na raslimali nyingi na umaskini kuendelea kuwepo yanatokana na kutoendelezwa kwa raslimali watu kwa lengo la watu kujitambua, kutambua wanachotaka na kusababisha kiwepo.
Alisema inasikitisha kuona kwamba watanzania wengi wanalalamika kuhusu hali ngumu kumbe ilhali wao huenda ndio wakawa sababu za matatizo hayo ya ukosefu wa maendeleo.
Alisema ni vyema watanzania wakajenga utamaduni wa kujisomea vitabu mbalimbali vinavyotoa mwanga wa kujituma na kuwajibika kwa kuwa vitabu hivyo vina tafiti nyingi za miaka mingi ambazo watanzania wakitumia kwa muda mfupi watafanya mabadiliko katika maisha yao.
Alisema uwapo kwa tafsiri ya Kiswahili kwa moja ya vitabu vyenye sifa kubwa duniani katika masuala ya menejimenti na ambacho kimekuwa katika 20 bora za vitabu duniani kwa miaka 20, kutasaidia watanzania wengi kujiangalia na kujifunza kuwa na dira na nidhamu ya kutekeleza yale ambayo wanayafikiria.
Alisema kwamba ari ya kusoma kazi mbalimbali kutasaidia watanzania kuwa na upeo mpana wa kujituma na kuwa na nidhamu ya malengo wanayostahili ya kufikia kwa muda mfupi na kwa ufanisi mkubwa.
Tafsiri hiyo ya kitabu ambayo imewezeshwa na Baraza la Kiswahili nchini Tanzania (BAKITA) na imeandaliwa taasisi ya ushauri wa masuala ya maendeleo ya raslimali watu (NFT).
NFT ambayo makao makuu yake yapo mjini Kampala, Uganda ina matawi Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini. Wajibu wake mkubwa taasisi hiyo ni kukabilina na changamoto mbalimbali za wafanyakazi kwa kutoa mafunzo yenye kutengeneza manufaa kwao na kwa menejimenti ya uhuru na kutegemeana katika kufanikisha maono ya taasisi husika.
Kutumika kwa kitabu hicho chenye kurasa 380 kwa kuangalia tabia zenye manufaa kunatokana na haja ya kubadilisha mfumo wa uongozi na ushirikishaji wenye lengo la kuchochea kutegemeana katika kuleta ufanisi.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kulia) na Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha ya Kiswahili, Vida Mutasa (wa pili kushoto) pamoja na wadau wengine wakifuatilia uchambuzi wa kitabu hicho.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na wageni waalikwa.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania ambapo alitoa rai kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu mbalimbali vinavyotoa mwanga wa kujituma na kuwajibika.
Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha ya Kiswahili, Vida Mutasa akielezea changamoto alizokutana nazo wakati wa kutafsiri kitabu hicho.
Pichani ni kikundi cha burudani kutoka Tanzania House of Talent (THT) wakitumia sanaa "Choreograph" kuzindua rasmi kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
Sasa kimezinduliwa rasmi.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akipokea kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kwa ajili ya mafunzo ya kuongeza manufaa binafsi na maeneo ya kazi kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege (kulia). Katikati anayeshuhudia tukio hilo ni Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha ya Kiswahili, Vida Mutasa
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akionyesha kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kwa ajili ya mafunzo ya kuongeza manufaa binafsi na maeneo ya kazi kwa waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani).
Kutoka kushoto ni Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Vida Mutasa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege, Mkurugenzi wa NFT Consult, Nambie Kiwanuka pamoja na Meneja biashara mkazi wa NFT Consult/Franklin Covey Tanzania, Joan Ajilong.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NFT Consult/Franklin Covey Tanzania.
Mratibu wa shughuli ya uzinduzi wa kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People"kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kutoka JB's PR & Events, Babbie Kabae akifafanua jambo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani).
Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa ambao ni maafisa rasilimali watu na wadau kutoka makampuni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :