Hatimae Bi Moza afanikisha kumpeleka mtoto wake India kwa matibabu
Posted in
Habari na Jicho Pevu la Kijiwe
No comments
Wednesday, June 10, 2015
By
danielmjema.blogspot.com
Bi Moza akiwa akimshindikiza
mtoto wake Moh'd Saidi,
Nchini India kwa matibabu
|
Bi Moza Moh'd Khamis anapenda tena kutoa shukurani za dhati kwa wale wote waliochangia kwa hali na mali kwa mtoto wake Moh'd Said Moh'd, kwenda kufanyiwa matibabu ya upandikizaji wa figo, nchini India.
Mapema asubuhi ya leo Bi Moza aliongea na blog ya swahilivilla ili kutoa taarifa kwa kukamilika safari yake ya kwenda nchini India pamoja na kutaka tumuombe Dua za kumtakia kila la kheri katika safari hiyo.
Moh'd Said Moh'd ameondoka leo Jumanne Juni 9, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuelekea Nchini India kwaajili ya matibabu yake.
Napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya Tanzania Bloggers Network (TBN) na waTanzania wote waishio Nchini Marekani, kumtakia kila la kheri Ndugu yetu Moh'd Said Moh'd katika matibabu yake huko Nchini India M/Mungu amjaalie wepesi katika safari yake na ampe afuweni na mafanikio katika mipangilio yote matibabu yake. Ameen.

Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :