HATIMAYE 18 WAPITA MCHUJO WA KWANZA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015
Posted in
Habari na Jicho Pevu la Kijiwe
No comments
Monday, June 8, 2015
By
danielmjema.blogspot.com
Baadhi ya Majaji wakijiandaa kutangaza Rasmi Matokeo ya washiriki 18 walioingia katia Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Kutoka kulia ni Dora Myinga Mkulima na Mjasiliamali, Mwandiwe Makame Mkulima na Mfugaji, Roselyn Kaihula kutoka Ekama Development
Meneja
Utetezi na Ushawishi wa Oxfam, Eluka
Kibona akiwakaribisha majaji kutangaza matokeo ya washindi
Zephaniah Muggitu a ambaye pia alikuwa ni Jaji Akieleza kwa ujumla Jinsi mchakato wa kuwapata washindi hao ulivyokuwa
Bw.
Jairos Mahenge ambaye Pia alikuwa ni Mmoja wa Majaji akizungumzia kwa
ufupi changamoto walizokutana nazo wakati wa Mchakato mzima wa kuhakiki
fomu za kuwapata washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula.
Ofisa
Mahusiano ya Ushawishi wa Oxfam Tanzania Suhaila Thawer akitoa maelezo
mafupi ya Jinsi watakavyo watembelea washindi 18 katika maeneo walipo
ili kuona shughuri zao na baadae kuwapata washiriki 15 ambao ndio
wataingia katika mshike mshike wa kumpata Mama Shujaa wa Chakula 2015
Dora
Myinga ambaye pia alikuwa ni jaji akiwataja washindi 18 walioingia
katika shindano la safari ya kumpata Mama shujaa wa Chakula
Baadhi ya majaji wakiwa wanaendelea na kazi wakati wa kuwatangaza washindi walioingia kuanza safari ya kumsaka Mama Shujaa wa Chakula 2015
*****
Baada ya zoezi la kupokea na kusahihisha fomu
za washiriki wa shindano la mama shujaa wa chakula 2015 kukamilika,
takribani washiriki 18 kutoka mikoa tofauti nchini wamefanikiwa kupita
katika mchujo wa kwanza kabla ya washiriki watatu kuyaaga mashindano
hayo na kubakia 15 ambao ndiyo wataingia kijijini kwa ajili ya kumpata
mshindi.
akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa
majaji waliohusika katika zoezi la kusahihisha fomu za washiriki,
Zephania Mugittu alisema kuwa idadi ya washiriki waliowasilisha fomu zao
ni 26,500 ambapo fomu zilizokidhi viwango zikiwa 2,317 tu.
Jaji
huyo aliongeza kuwa fomu za washiriki 21 ndiyo zilizovuka alama zaidi
ya asilimia hamsini huku vigezo vya umri, shughuli za kilimo cha mazao
ya chakula, uvuvi na ufugaji vikiwabakiza washiriki 18 wenye alama za
juu kutoka mikoa tofautitofauti.
Naye Ofisa Mahusiano ya Ushawishi wa Oxfam Tanzania
Suhaila Thawer alimalizia kwa kusema washiriki 18 wote watatembelewa
maeneo waliyopo kuhakikisha kama wanafanya kazi hizo kweli na baadae
kuanza rasmi mchakato wa kumpata Mama Shujaa wa Chakula 2015.
Washiriki hao 18 ni Getrude Bundala Deonatus(35) Ukerewe Mwanza, Winnie L. Mallya (24) Kilimanjaro Moshi, Dina Samwel
Sumari (62) Meru Arusha, Tatu Ramadhani Kilua (48) Lushoto Tanga, Edna Gabriel
Kiogwe (40) Ilala Dar es salaam, Neema Hilonga (35) Hanang Manyara, Pili Kashinje Itamba (30) Kaskazini(U), Eva
Mageni Daudi (31) Bagamoyo Pwani, Hawa Athumani
Mkata (56) Masasi Mtwara, Wandutha Daud Kitoelth (48) Mkalama Singida,
Shida Daudi Mwedugo (35) Chamwino Dodoma, Hellen Materu (36) Iringa Mjini,
Upendo Paulo Mhomisoli (35) Njombe, Savera
Xeveri Mutahyabarwa (65) Bukoba Mjini Kagera, Carolina Humphrey Chelele (48) Kilombero Morogoro, Stella Fabian Masulya (42) Ukerewe Mwanza, Regina Kapili Stephano (19) Mpanda Katavi, Rehema Daniel Lukali (46) Sumbawanga Rukwa.
WEKEZA KWA WAKULIMA WANAWAKE WADOGO WADOGO INALIPA
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :