MBOWE: TUMEKUBALIANA NA DKT. SLAA APUMZIKE KIDOGO

Posted in
No comments
Monday, August 3, 2015 By danielmjema.blogspot.com

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Mbowe-Tumekubaliana na Katibu Mkuu apumzike kwa muda, kwamba sis tuendelee na atakapokuwa tayari ataungana nasi mbele ya safari. Akihutubia Kikao cha Baraza Kuu leo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema, tumekubaliana na Katibu Mkuu apumzike kwa muda, kwamba sisi tuendelee na atakapokuwa tayari ataungana nasi mbele ya safari.

Mbowe-Chama hiki hatukiendeshi kwa siri, tunakiendesha kwa mikakati. amesema walilazimika kutumia kila mbinu halali ambayo inakiwezesha chama chetu kusaka matumaini na matarajio ya wananchi. Aidha Mwenyekiti huyo wa Chadema amesema walijiridhika pasipo shaka kwamba ugeni wa Edward Lowassa katika chama ni mpango wa Mungu.

Mbowe amewahakikishia wanachama na wajumbe wa Baraza kuu kuwa wako imara huku wakiamini kuwa Umoja wao ndio ushindi na kuongezaq kuwa fursa iliyojitokeza ni nadra.

Mbowe amesema kuwa Mtikisiko uliojitokeza ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) umekuja kipindi ambacho Watanzania wanamatamanio ya mabadiliko na kuongeza kuwa kamwe Chadema hakiwezi kuendelea kuwa chama cha kuendelea kuhubiri mabaya ya jana tukashindwa kuhubiri maendeleo ya kesho.

Akihutubia Mkutano huo unaondelea muda huu, Jijini Dar es salaam, Mbowe amesema Kipigo wanachopata CCM, hawajawahi kukipata tangu siasa za vyama vingi vianze huku akiendelea kusisitiza kwamba Chadema itaendelea kumpokea kila kumpokea kila wanayeweza kumpokea vyama vilivyo nje ya UKAWA kwani ni imani yao kuwa Mungu ameamua kuitumia Chadema kujeruhi na kuangusha CCM.

Mwenyekiti huyo amesisitiza kuwa CHADEMA ni chama cha siasa, ni chama makini, na kwamba chama makini ni chama cha watu, chama kisichokuwa makini ni chama cha viongozi.


Kwa hisani ya JF

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .