TFDA YATOA TAHADHARI YA KUWEPO KWA VIPODOZI VYENYE VIAMBATO VILIVYOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI

No comments
Tuesday, August 18, 2015 By danielmjema.blogspot.com


 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya TFDA Dar es Salaam leo, wakati akitoa tahadhari ya uwepo katika soko wa vipodozi vyenye viambato vilivyopigwa marufuku na Serikali. Kulia ni Mkurugenzi wa Dawa  na Bidhaa Nyongeza, Fimbo Mitangu.
 Mkurugenzi wa Dawa  na Bidhaa Nyongeza, Fimbo Mitangu (kushoto), akizungumza katika mkutano huo huku akionesha moja ya kopo lenye kipodozi vilivyopigwa marufuku. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uendelezaji Huduma wa TFDA, Chrispin Severe 
 Mkurugenzi wa Usalama wa chakula, Raymond Wigenge (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Maabara wa TFDA, Charys Ugullam (kulia), wakiwa kwenye mkutano huo na wanahabari.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.



1.            MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) ni Wakala wa Serikali ulio chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wenye jukumu la kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa aina ya chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.

2.            TFDA inautaarifu umma kuwa kupitia mfumo wake wa ufuatiliaji ubora na usalama wa bidhaa kwenye soko, imebaini uwepo wa vipodozi vyenye viambato vilivyopigwa marufuku aina ya “steroids” zinazojulikana kitaalam kama “clobetasol propionate”, “hydrocortisone” na “triamcinolone”.

3.            Jumla ya Vipodozi aina tofauti 36 vya jamii ya krimu (creams) na losheni (lotion) vimebainika kuwa na viambato hivyo vilivyopigwa marufuku baada ya kufanya uchunguzi wa kina wa matoleo 57 yaliyochukuliwa kwenye soko na viwanda vilivyotengeneza.

4.            Vipodozi hivyo vimetengenezwa na makampuni manne (4) yaliyoko hapa nchini na kiwanda kimoja (1) kilichoko nje ya nchi kama ifuatavyo:-

Na.
Jina la kiwanda
Idadi ya vipodozi
Idadi ya matoleo
1.
Chemi & Cotex Industries Limited - Dar es Salaam
6
7
2.
Mamujee Products Limited - Tanga  
11
20
3.
Tanga Pharmaceutical & Plastics Limited - Tanga
15
24
4.
Tridea Cosmetics Limited - Dar es Salaam
3
5
5.
Johnson & Johnson (Pvt) Ltd, Rattray Road, East London, South Africa
1
1

Jumla
36
57

5.            Steroids aina ya “clobetasol propionate”, ‘hydrocortisone’’ na “triamcinolone” hutumika kama dawa kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi yajulikanayo kitaalam kama eczema, herpes labialis, psoriasis, contact dermatitis, alopecia areata, vitiligo, lichen sclerosus, lichen planus na mycosis fungoides. Steroids hizi hazitakiwi kutumika zaidi ya wiki mbili na lazima mgonjwa apate ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa hizi.

6.            Baadhi ya madhara yanayotokana na kutumia dawa hizi ni pamoja na muwasho na kuvimba kwa ngozi (allergic contact dermatitis), ngozi kuwaka moto (burning sensation), ngozi kukatikakatika (skin cracking), ngozi kubabuka (fissuring) ngozi kukosa chembembe aina ya melanin inayoleta kinga na hivyo kuifanya ngozi kuwa nyeupe isivyo kawaida (hypopigmentation), madhara kwenye mifupa (osteoporosis), kizunguzungu (dizziness), ngozi kukauka (skin dryness), shinikizo la damu kwenye macho (glaucoma), vinyweleo vya ngozi kupata athari (folliculitis), kuwashwa mara kwa mara (excessive itching, pruritus, erythema and irritations), vidole kufa ganzi (numbness of fingers), ngozi kusinyaa (skin atrophy) na ngozi kubanduka (skin peeling/maceration). Madhara mengine ni pamoja na ngozi kuwa nyekundu (skin redness), kusikia kichefuchefu (nausea), kichwa kuuma (headache), kushindwa kupata usingizi (insomnia), kutoka jasho jingi (sweating), kupata chunusi kubwa kwenye ngozi (acne), kuchoka (fatigue), kuongezeka uzito (weight gain), mapigo ya moyo kutoenda sawa (uneven heartbeats) na kuona maluweluwe (blurred vision).

7.            Kufuatia hali iliyojitokeza na kwa kuzingatia madhara yanayoweza kusababishwa na matumizi ya steroids kwa muda mrefu, TFDA imechukua hatua zifuatazo:

a.      Kuzuia kwa muda wa miezi sita (6) utengenezaji wa vipodozi aina ya krimu, losheni na jeli kwenye viwanda vinne (4) vilivyohusika.
b.      Kuwaelekeza wenye viwanda vilivyohusika kuviondoa vipodozi vilivyokutwa na steroids kwenye soko na kuviteketeza kwa gharama zao wenyewe.
c.       Kufuta usajili wa vipodozi 31 vilivyokuwa vimesajiliwa.
d.     Kuwaelekeza Mameneja wa Ofisi za Kanda za TFDA kufanya ukaguzi katika maeneo yao kwa kushirikiana na Ofisi za Halmashauri ili kuondoa katika soko vipodozi vyote vilivyohusika.

8.            Pamoja na hatua hizo, TFDA inatoa maelekezo yafuatayo:-

a.      Wananchi wote wasitumie vipodozi husika kwa kuwa vina madhara ya kiafya. Wananchi wanaaswa kuangalia lebo za vipodozi walivyonavyo majumbani na wakiona vina majina yaliyoainishwa waache kutumia vipodozi hivyo mara moja.
b.      Wasambazaji na wauzaji wote kurudisha vipodozi vilivyohusika kwa watengenezaji au kwa waliowauzia ili hatua za uteketezaji ziendelee.

9.            TFDA inaendelea kufuatilia vipodozi vingine vyote ili kujiridhisha na ubora na usalama wake kwa watumiaji. Vile vile itaendelea na kazi yake iliyopewa ya kulinda na kudumisha afya ya jamii kwa kuhakikisha bidhaa aina ya chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba zinazotengenezwa hapa nchini au kuingizwa kutoka nje ya nchi ni bora, salama na zenye ufanisi unaotakiwa.

10.        TFDA itawachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaojihusisha na uvunjaji wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219 na inawaomba wananchi wote kuendelea kutoa taarifa pale wanapobaini uwepo wa bidhaa (chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba) duni au bandia kwenye soko la Tanzania. 


ORODHA YA VIPODOZI VILIVYOBAINIKA KUWA NA VIAMBATO VILIVYO PIGWA MARUFUKU




Na.
Jina la kipodozi
Namba ya usajili
Toleo
Tarehe ya kuishamatumizi
Sehemusampuliilipochukuliwa
Aina ya kiambatokilichokutwa

Chemi&Cotex Industries Limited, Dar es Salaam
1.    
Lovely Body Cream - Lemon
TAN15 CP 0095
12&16
Feb-18
Kwenye soko&Kiwandani
ClobetasolProprionate
2.    
Baby Soft Body Lotion
Haijasajiliwa
08
Dec-16
Kwenye soko
ClobetasolProprionate
3.    
Siri Moisturizing  Cream- Cocoa Butter
TAN13 CP 3118
26
Jan-18
Kiwandani
ClobetasolProprionate
4.    
Siri Moisturizing  Cream- Lemon
TAN13 CP 3120
03
May- 18
Kiwandani
ClobetasolProprionate
5.    
Lovely Body Cream - Lemon
TAN15 CP 0094
16
Mar-18
Kiwandani
ClobetasolProprionate
6.    
Lovely Body Cream - Papaya
TAN15 CP0096
10
May-18
Kiwandani
Hydrocortisone

Mamujee Products Limited, Tanga
7.    
Beauty Care Aloe Vera Beauty Cream
Haijasajiliwa
00283
Sep-15
Kwenye soko&Kiwandani
ClobetasolProprionate
8.    
BOSS Hand & Body Lotion
TAN 15 CP 0300
10/0077258

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .