LEO JANUARI 8,NI SIKU YA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA KWA MWANZILISHI NA MMILIKI WA MALUNDE1 BLOG,IJUE HISTORIA YAKE HAPA
Posted in
Habari na Jicho Pevu la Kijiwe
No comments
Friday, January 8, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
MENEJIMENTI
na Wafanyakazi wa Malunde1 blog,kwa bashasha wanatoa salamu za pongezi
kwa mwanzilishi wa Malunde1 blog,Fahari ya Shinyanga ndugu Kadama
Malunde kwa kujaaliwa , leo Januari 08,2016;kuadhimisha siku ya
kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Kadama
Malunde aliyelelewa na wazazi wake kwa maadili ya kabila la Kisukuma
ndiye mwanzilishi pia Mmiliki wa Malunde1 blog, alizaliwa katika kijiji
cha Zobogo wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga miaka kadhaa iliyopita.
Wazazi wake waliamini kuwa elimu ndiyo urithi pekee utakaomfaa mtoto wao.
Mwaka
1995 alianza safari yake ya kujipatia Elimu,kwa kuanza darasa la kwanza
katika Shule ya Msingi Bugisi wilaya ya Shinyanga,hadi mwaka 2001
alipohitimu Elimu hiyo ya msingi.
Mwaka
2002 hadi 2005,alijiunga katika shule ya sekondari Kituli iliyopo
wilayani Shinyanga kwa masomo ya kidato cha Kwanza hadi Nne;ndipo
alipojiunga katika shule ya sekondari Ngudu iliyopo mkoani Mwanza kwa
masomo ya kidato cha Tano na Sita mwaka 2006/2008.
Mwaka
2008/2011 alijiunga katika shule kuu ya Uandishi wa Habari na
Mawasiliano ya Umma(SJMC) katika chuo kikuu cha Dar es salaam kwa ajili
ya masomo ya Uandishi wa Habari(BA In Journalism).
Tangu
mwaka 2009 Kadama Malunde amekuwa akifanya kazi katika vyombo mbalimbali
vya habari,vikiwemo Mlimani Radio,Kahama fm,Radio Faraja Fm,Gazeti la
The Hill Observer,Zanzibar leo na Mtanzania,ambapo katika baadhi ya
vyombo vya habari aliwajibika katika nyadhifa za Mhariri wa
Habari,Mtangazaji na Mwandishi wa Habari.
Mbali
na kuwajibika kwa nyakati kadhaa katika vyombo hivyo vya habari,amemudu
kuanzisha na kutumia muda mwingi zaidi kuendesha mtandao wa kijamii wa www.malunde1.blogspot.com pamoja na kuandikia gazeti la Mtanzania.
Aidha
Kadama Malunde mwenye makazi yake mjini Shinyanga ni mwanachama wa
Mtandao wa wamiliki wa blogu Tanzania(Tanzania Bloggers Network-TBN)
lakini pia ndiye mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa
Shinyanga(Shinyanga Press Club-SPC) tangu mwezi Julai 2015.
Malunde,
Pamoja na kujivunia mafanikio yake kitaaluma lakini bado anazo ndoto
nyingi katika taaluma yake na hiyo inampelekea kuamini kuwa bado
anahitaji kuongeza nguvu katika kuifikia jamii hasa ya watu wa pembezoni
ambayo inayokabiliwa na matatizo mbali mbali.
Tunamtakia
kila la kheri katika kusherekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake,Mwenyezi
Mungu amjaalie umri mrefu,siha maridhawa,hekima na mafanikio katika
maisha yake.
Happy Birth day Brother!!
Tumekuletea baadhi ya picha za Kadama Malunde,katika matukio mbalimbali
Hapa ni katika studio ya Mlimani Radio jijini Dar es salaam Kadama Malunde akifanya kipindi cha radio mwaka 2011.
Mwaka 2012,Kadama Malunde akisoma Habari katika studio ya Radio Faraja FM Stereo ya mkoani Shinyanga.
Mwaka 2015 Kijana Kadama Malunde katika pozi
Kadama Malunde akiwa na mmoja wa wakimbiza mbio za mwenye mkoani Shinyanga mwaka 2014
Kadama Malunde akiwajibika mtaani na mwandishi wa Malunde1 blog,bwana Marco Maduhu
Kadama Malunde akiwa na msanii wa maigizo na vichekesho Senga
Mwaka
2015 Kadama Malunde alipokutana na msanii maarufu wa nyimbo za asili
ambaye huimba kwa lugha ya Kisukuma Bhudagala Mwanamalonja ,akiwa katika
harakati zake za kutafuta nyimbo za wasanii wa nyimbo za asili aziweke
katika mtandao wake wa Malunde1 blog,kupitia kipengele cha NYIMBO ZA
ASILI.
Kadama Malunde akiwa na msanii Bhudagala Mwanamaonja
Kadama
Malunde akiwa na msanii Bhudagala Mwanamalonja katika show ya msanii
huyo katika kijiji cha Usanda kata ya Samuye wilaya ya Shinyanga
Kadama Malunde akisalimiana na katibu mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania(MCT) Kajubi Mukajanga.
Akiwa katika pozi.
Akiwa katika mizunguko yake.
Akichat.
Katika pozi.
Akiwa
na mwenyekiti mstaafu wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
ndugu Shija Felician(baada ya Shija,Kadama ndiyo mwenyekiti mwingine wa
klabu hiyo).
Akiwa Mikumi mkoani Morogoro wakati wa ziara zake mwaka 2015.
Kadama
Malinde akiwa katika pozi na waandishi wa habari Philipo Malaki (RFA)na
Veronica Natalis( Radio Faraja/DW) ambao hufanya kazi kwa ukaribu zaidi
na Malunde1 blog.
Kadama Malunde akiwajibika katika ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga hivi karibuni.
Kadama Malunde akiwa ofisini kwake
Kadama
Malunde akiwa katika ziara yake kutembelea bwawa la Ning'wa ambalo ni
moja ya vyanzo vya maji katika manispaa ya Shinyanga.
Kadama
Malunde akiendesha mkutano wa wadau wa habari mkoani Shinyanga siku
chache kabla ya uchaguzi mkuu 2015 nchini,wakijadili namna ya
kuhakikisha amani ya nchi inakuwepo kabla,wakati na baada ya uchaguzi wa
madiwani,wabunge na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Kadama Malunde akiwa na rais wa waandishi wa habari Tanzania Deo Nsokolo.
Kadama
Malunde akiwa na baadhi ya Bloggers nchini Tanzania,kulia kwake ni
mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa Blogu nchini(TBN) bwana Joachim
Mushi walipokutana katika mkutano wa kwanza mwaka 2015.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :