BURUNDI: WANAJESHI 100 KUPELEKWA BURUNDI

No comments
Sunday, February 28, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Umoja wa Afrika umetangaza kwamba utawapeleka waangalizi 100 wa haki za kibinaadamu pamoja na waangalizi wengine 100 wa kijeshi nchini Burundi.

Umesema kuwa rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza ameunga mkono mpango huo. Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma aliongoza ujumbe wa viongozi watano wa Afrika katika ziara ya siku mbili wiki hii.

Walikutana na bwana Nkurunziza na viongozi wawili wa upinzani ambao wamesalia nchini humo hata baada ya ghasia zilizozuka mwezi Aprili baada ya Nkurunziza kutangaza kuwa atawania muhula wa tatu. Wamesema kuwa mpatanishi wa AU rais Museveni wa Uganda ataanzisha mazungumzo hivi karibuni.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .