KENYA: RUBANI ADAIWA KUMDHALILISHA POLISI WA KIKE

No comments
Tuesday, February 23, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Polisi nchini Kenya wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kisa ambapo rubani wa ndege iliyombeba Naibu Rais William Ruto anadaiwa kumdhalilisha afisa wa polisi wa kike.

Kisa hicho kilitokea Jumapili wakati Bw Ruto alikuwa amezuru mji wa Ndunyu Njeru, jimbo la Nyandarua katikati mwa nchi hiyo.

Video iliyochukuliwa na mmoja wa walioshuhudia kisa hicho imesambaa sana mtandaoni watu wakitaka hatua zichukuliwe dhidi ya rubani huyo.

Kwenye video hiyo, rubani huyo anaonekana akimkaripia mwanamke huyo ambaye wakati huo anatumia simu, kumpokonya bakora yake na kicha majibizano yanatokea. Muda mfupi baadaye, rubani huyo anaonekana akimsukuma afisa huyo wa polisi.

Mkuu wa polisi Joseph Boinnet, kupitia taarifa, ameagiza maafisa wa polisi kuanzisha uchunguzi mara moja kuhusu kisa hicho na pia akamtaka rubani huyo kujisalimisha kwa polisi. Afisa wa mawasiliano wa Bw Ruto, Bw David Mugonyi, amesema kiongozi huyo amefahamishwa kuhusu kisa hicho.

“Naibu Rais amewaagiza polisi kuchukua hatua mara moja. Naibu Rais anaheshimu polisi wetu wenye bidii ambao hufanya kazi saa nyingi kulinda nchi. Kisa hiki hakikubaliki, na ni cha kusikitisha na nimewataka polisi kuchunguza kitendo hicho cha rubani huyo,” taarifa yake imesema.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .