BURUNDI: BAN KI-MOON KUKUTANA NA RAIS NKURUNZIZA
Posted in
afrika mashariki
No comments
Tuesday, February 23, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki Moon amepangiwa kukutana na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza katika
juhudi za kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo.
Bw Ban, aliyewasili nchini Burundi Jumatatu, atakutana na Bw
Nkurunziza leo ikulu ya rais na baadaye wawili hao wanatarajiwa kutoa
taarifa ya pamoja.
Baada ya kuwasili Jumatatu, Bw Ban alikutana na wawakilishi wakuu wa vyama vya siasa na kujadili amani na usalama. Mamia
ya watu wameuawa na maelfu kutoroka makwao tangu kuanza kwa machafuko
nchini humo mwezi Aprili mwaka jana baada ya Rais Nkurunziza kutangaza
angewania urais kwa muhula wa tatu.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, na viongozi wengine wanne wa nchi
za Afrika wanatarajiwa kufika Burundi mnamo Alhamisi kinachoonekana kuwa
juhudi za viongozi wa bara Afrika kuongeza shinikizo kwa Bw Nkurunziza
kufanikisha mazungumzo ya kutafuta amani.
Watakaosaidiana na Rais Zuma ni pamoja na Rais wa Gabon Ali Bongo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn. Bw
Zuma amesema Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekuwa akiongoza
mazungumzo ya amani kwa niaba ya kanda lakini viongozi hao watawakilisha
Umoja wa Afrika.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :