UGANDA: BESIGYE AKAMATWA TENA!
Posted in
afrika mashariki
No comments
Friday, February 19, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Wanajeshi wa Uganda wakishirikiana
na maafisa wa polisi wamevamia na kuzingira afisi za chama cha upinzani
za Forum for Democratic Change (FDC).
Kiongozi wa chama hicho, Dkt
Kizza Besigye, ambaye amekuwa akiwania urais amekuwemo ndani ya afisi
hizo na mwandishi wa BBC Patience Atuhaire anasema polisi wameondoka
naye akiwa kwenye gari lao.
Kituo cha televisheni cha NBS
kimeripoti kuwa Besigye na rais wa FDC Mugisha Muntu wamekamatwa katika
makao makuu hayo eneo la Najjanankumbi, na wafuasi wa chama hicho
wakatawanywa kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi.
Mgombea mwingine wa
urais Amama Mbabazi amepakia video kwenye Twitter inayoonesha maafisa wa
usalama nje ya nyumba yake. Anasema polisi wameanza kuwakamata watu nje
ya nyumba yake. Viongozi wa chama cha FDC walikuwa wakijiandaa kuhutubia wanahabari kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika jana.
Maafisa
wa usalama wanashika doria kwa wingi maeneo yanayozunguka makao makuu
hayo ya chama cha FDC, mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga anasema.
Milio inasikika ingawa haijabainika iwapo ni ya risasi halisi, risasi za mipira au mabomu ya kutoa machozi.
Hii ni mara ya tatu kwa Dkt Besigye kukamatwa wiki hii.
Alikamatwa jana jioni katika kitongoji cha Naguru, mjini Kampala katika nyumba ambayo upinzani ulidai wizi wa kura ulikuwa ukifanyika.
Jumatatu, alizuiliwa kwa muda wakati akifanya kampeni mjini Kampala. Polisi walisema alijaribu
kupitia barabara isiyoruhusiwa.
Habari Zingine
- Wachimbaji mgodi 15 waliokwama ardhini waokolewa nchini Tanzania
- Al-Shabab washambulia kambi ya majeshi ya Kenya nchini Somalia
- UHURU WA HABARI SIO KUIANGALIA TU SERIKALI - MWAKYEMBE
- JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA LATANGAZA KUSUSIA KUANDIKA HABARI ZA MKUU WA MKOA WA DAR
- WENGI WALIVYOJITOKEZA KUMUAGA MWANA TBN JENNIFER LIVIGHA (CHINGA ONE) HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :