RIPOTI YA DUNIA YAITAJA SERIKALI YA RWANDA KUONGOZA KWA UTENDAJI AFRIKA MASHARIKI
Rwanda imeorodheshwa kuwa nchi ya 7 duniani kwa kutoa huduma za
haraka na rahisi za serikali. Ripoti iliyotolewa na baraza la Uchumi
duniani imeiorodhesha Rwanda mbele ya Malaysia, Uswisi na Luxembourg
ambazo zilichukua nafasi za 8, 9 na 10.
Utafiti wa baraza hilo pia
umeonesha kuwa serikali ya Qatar ndio iliyo na utendaji bora zaidi
ikifuatiwa na Singapore na Finland.
Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi wa Bodi ya utawala ya
Rwanda Bwana Anastase Shyaka amesema nchi yake inafanya juhudi kubwa
kukuza uwazi na uwajibikaji kwenye mfumo wake, na raia wengi wana habari
kuhusu jinsi serikali inavyofanya kazi na kutoa maamuzi.
Kwingineko
barani Afrika Mauritius iko kwenye nafasi ya 26 na kama Afrika Kusini
iko katika nafasi ya 32 Kenya na Tanzania Je?
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :