TANZANIA: MAGUFULI ATEUA WAKUU 13 WAPYA WA MIKOA

No comments
Sunday, March 13, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Rais wa Tanzania amewateua wakuu 13 wapya wa mikoa miongoni mwa orodha mpya ya wakuu 26 wa mikoa iliyotangazwa leo na ikulu ya rais.


Rais John Pombe Magufuli amewahifadhi wakuu 13 waliohudumu katika serikali ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huo umetangazwa na katibu mkuu kiongozi, Balozi Mhandisi John William Kijazi

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari iliyotiwa sahihi na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, katika ikulu, Gerson Msigwa, Viongozi hao wote walioteuliwa wataapishwa katika hafla maalum itakayoandaliwa jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa tatu asubuhi jijini Dar es salaam.


Orodha ya wakuu wa mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

Paul Makonda Dar es Salaam
Ezekiel Elias Kyunga Geita
Salum Mustafa Kijuu Kagera
Raphael Muhuga Katavi
Emmanuel Maganga Kigoma
Godfrey Zambi Lindi
Dkt. Steven Kebwe Morogoro
Zerote Steven Rukwa
Anna Malecela Kilango Shinyanga
Methew Mtigumwe Singida
Antony Mataka Simiyu
Aggrey Mwanri Tabora
Martine Shigela Tanga
Jordan Mungire Rugimbana Dodoma
Said Meck Sadick Kilimanjaro
Magesa Mulongo Mara
Amos Gabriel Makalla Mbeya
John Vianey Mongella Mwanza
Daudi Felix Ntibenda Arusha
Amina Juma Masenza Iringa
Joel Nkaya Bendera Manyara
Halima Omary Dendegu Mtwara
Dkt. Rehema Nchimbi Njombe
Evarist Ndikilo Pwani
Said Thabit Mwambungu Ruvuma
Chiku Galawa Songwe (Mkoa mpya)

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .