Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa bwana Kofi Annan amemkosoa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kwa
kuwania muhula wa tatu. Bw Annan amesema Nkurunziza anafahamu
vyema kuwa ni kinyume cha katiba ya taifa hilo kuwania madaraka kwa
zaidi ya vipindi viwili.
Raia huyo wa Ghana anamlaumu rais Nkurunziza kwa kusababisha maandamano yaliyosababisha vifo vya takriban watu mia nne. Bw
Annan ameiambia BBC kuwa bw Nkurunziza haoneshi dalili zozote za
kutafuta suluhu la amani wala nia ya kutaka mazungumzo ya kweli na
wapinzani wake.
Katibu huyo wa zamani ameiomba jamii ya imataifa kuyasaidia mataifa
ya Afrika yanayokabiliwa na matatizo chungu nzima kama vile Ethiopia
inayokabiliwa na baa la nja. Annan anasema kuwa mataifa hayo ya
Afrika yamesahaulika huku kurunzi ya ulimwengu ikiangazia Syria na
mataifa ya Mashariki ya kati.

No comments:
Post a Comment