Wapiganaji wa kundi la waasi wa FDLR washambulia kituo cha polisi nchini Rwanda. Jeshi
la Rwanda limethibitisha kuwa kituo kimoja cha polisi cha eneo la
Bugeshi ,Kaskazini Magharibi kwenye mpaka kati ya nchi hiyo na Jamuhuri
ya Kidemokrasia ya Congo kimeshambuliwa na wapiganaji wa kundi la FDLR.
Kulingana
na naibu msemaji wa jeshi la Rwanda Luteni kanali Rene
Ngendahimana, wapiganaji wanaokadiriwa kuwa kati ya 20 na 30 wa FDLR
wamevuka eneo hilo la mpakani mnamo usiku wa manane kuamkia leo na
kushambulia kituo hicho cha polisi.
Hata hivyo hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu idadi ya
waliokufa au kujeruhiwa katika shambulio hilo,ila katika tanganzo
linalopatikana kwenye ukurasa wa twitter wa jeshi la Rwanda,naibu
msemaji wa jeshi amesema kuwa jeshi la Rwanda linadhibiti eneo hilo na
kwamba taarifa zaidi kuhusu shambulio hilo zitatolewa baadaye.
Mwezi
uliopita,eneo hilo pia lilishambuliwa na wapiganaji waliotajwa kuwa wa
kundi la FDLR ambapo taarifa ya jeshi la Rwanda ilisema kuwa mpiganaji
mmoja wa FDLR aliuawa.
BBC SWAHILI

No comments:
Post a Comment