BARCELONA KUKUTANA NA KILICHOIKUTA MALLORCA 1998/99?
Mnamo
March 20, kikosi cha Luis Enrique kikiwa kinaongoza 2-0 vs Villareal,
kikaruhusu wapinzani wao warudi mchezoni na kusawazisha magoli yote
katika mchezo uliopigwa katika dimba la Estadio El Madrigal. Wakati huo ilionekana ni kosa dogo Barca wamefanya na halitokuwa na athari kubwa katika mbio zao za ubingwa.
Hakuna ambaye aliyapa umuhimu mkubwa matokeo ya mechi ile. Mechi zilizofuatia mbili za Wakatalunya hazikuwa nyepesi, walikuwa
wanakutana na Real Madrid CampNou, kisha kufunga safari kwenda Estadio
de Anoeta kucheza vs Real Sociedad.
Hata hivyo, kila mtu alitabiri Barca wangewaadhibu vijana wa Zinedine
Zidane, na ilikuwa muda wa muafaka kwa Luis Enrique kulipa kisasi dhidi
ya Real Sociedad baada ya kufungwa msimu na kidogo aikose kazi yake.
Haikuwa rahisi kama ilivyoadhaniwa, Barca wakapoteza mechi zote mbili na tangu hapo mambo yakazidi kuharibika. Wakati Valencia walipoenda Camp Nou miezi miwili iliyopita, Barcelona
waliwafunga magoli 7 katika nusu fainali ya Copa del Rey na kuelekea
mchezo wa jana jumapili Barca walipewa nafasi ya kuweza kurejea katika
kiwango chao.
Barca walionekana kuimarika katika mchezo wa jana, lakini walikuwa ni
Valencia waliorudi kwenye ubora wao ambao walihakikishia Barcelona
anaangukia pua kwene mchezo wa 3 mfululizo wa ligi, mara ya kwanza tangu
mwaka 2003.
Kinachoikuta
Barcelona msimu huu, kinaelekea kufanana na kilichoikuta Real Mallorca
msiku wa 1998/99, Real Mallorca walipoteza uongozi wa pointi 9 na
kuiacha Barcelona ya Louis Van Gaal kwenda kushinda ubingwa wa ligi
msimu huo.
Huku kukiwa kumebakiwa mechi 5 kabla ya msimu kumalizika – kwa hakika
Barcelona hawatotaka kupata matokeo mabaya tena, wanaweza kujikuta
wamegeuka Real Mallorca ya msimu wa 1998/99 na Atletico au Real Madrid
wakawa Barca ya msimu huo, kwa kutwaa La Liga baada ya kuachwa nyuma kwa
pointi nyingi na viongozi wa ligi kabla ya kuwafikia na kuwazidi.
SOURCE: http://shaffihdauda.co.tz
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :