CHRIS BROWN AFUNGUKA ALIVYOTAKA KUJIUA KWA SABABU YA RIHANNA
Posted in
Burudani
No comments
Tuesday, April 19, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Mwanamuziki Chris Brown amesema kuwa
alitaka kujiua baada ya kumshambulia aliyekuwa mpenziwe Rihanna kabla
ya tuzo za Grammy mwaka 2009. Katika kipande kifupi cha makala
yake ya 'Karibu katika maisha yangu',mwanamuziki huyo wa mtindo wa R
& B amesema kuwa uhusiano wao ulikuwa kama ndoto lakini akajihisi
kama hayawani.
''Nilikuwa katika kilele cha dunia, nyimbo zangu zikiongoza, nikapendwa na wengi nchini Marekani kabla ya kuanguka hadi kuwa adui wa uma'',alisema. Brown alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kufuata shambulio hilo.
Kifungo hicho kilisitishwa mwaka jana baada ya jaji moja kusema kuwa nyota huyo amekamilisha mahitaji yake yote na kufunga kesi hiyo rasmi. Makala hiyo inayowaonyesha Jennifer Lopez,Usher,Mike Tyson,Jamie Fox na Rita Ora,Chris Brown anasema kuwa ''Nilihisi kama nyota ,lakini nilijiharibia''. ''Nilikuwa nikilala.Sikuweza kula,nilijihisi maarufu'',alikiri.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :