Kenya sasa inataka faili za kesi
zinazowakabili wakenya watatu wanaotuhumiwa kuingilia ushahidi wa
mashahidi wa ICC kushtakiwa nchini humo. Mwanasheria mkuu Profesa
Githu Muigai amesema kuwa Kenya ina mahakama zilizo na uwezo za kushtaki
kesi ndogo kufuatia kuanguka kwa kesi kuu iliowahusisha wakenya sita
maarufu kama Ocampo 6.
Mwanasheria huyo pia ameshtumu idara ya
mashtaka katika mahakama ya ICC kwa kushindwa kushirikiana na Kenya
kuhusu ombi la awali lililowasilishwa kwa aliyekuwa kiongozi wa mashtaka
Moreno Ocampo kuikabidhi Kenya faili zote za washukiwa.
Amesema kuwa Kenya ina haki ya kushirikiana na mahakama hiyo au la iwapo ICC itafeli kuikabidhi Kenya faili hizo. Ameongezea
kuwa mpango wa Kenya kujiondoa katika mahakama hiyo utaangaziwa na
Umoja wa Afrika AU na kwamba Kenya kama taifa haijaanza harakati za
kujiondoa.

No comments:
Post a Comment