Kenya imeilaumu
Tanzania kwa kuwaweka raia wa Ethiopia katika eneo lake la mpaka siku ya
Jumanne badala ya kuwarudisha makwao kulingana na ripoti ya gazeti la
The standard nchini Kenya. Raia hao wa Ethiopia walikuwa wamewachiliwa huru baada ya kuhudumia vifungo vya mashtaka tofauti ya uhalifu nchini Tanzania.
Maafisa wa polisi wameagizwa kutowaruhusu wageni hao kuingia nchini Kenya. ''Watarudishwa
nchini Tanzania walikotoka.Kisa hicho hakikubaliki na hakiruhusiwi na
sheria'',Afisa wa Kenya Henry Wafula alinukuliwa akisema.

No comments:
Post a Comment