KIGALI: TANZANIA NA RWANDA ZAFUNGUA UKURASA MPYA YA UJIRANI MWEMA
Mataifa wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki, Rwanda na Tanzania zimeahidi kushirikiana zaidi kibiashara katika ukurasa mpya wa uhusiano baina ya mataifa hayo jirani. Hayo yamewadia katika mkutano wa rais wa Rwanda Paul Kagame na mgeni wake rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Marais
hao wameyasema hayo leo mnamo mwanzo wa ziara ya rais Magufuli nchini
Rwanda ambayo ndiyo ziara yake ya kwanza kuchaguliwa kwake mwaka
uliopita. Maneno ya undugu,urafiki ,uhusiano mwema na uhusiano
imara yametamkwa sana na viongozi hawa,Rais Kagame akisisitiza ndio
ndiyo msingi mkubwa wa kujenga nchi hizi mbili.
Ziara hiyo ya siku
mbili inaangaliwa na wengi kama ya kufungua ukurasa mpya wa uhusiano
kati ya nchi hizo mbili baada ya kipindi Fulani cha uhusiano baridi. ''Mnajua vyema kuwa mimi sipendi kusafiri, kwa sababu ninapenda kubana matumizi. ''Nimealikwa sehemu nyingi hata ulaya nimealikwa lakini bado sijaenda. ''Lakini nilipoalikwa na rais kagame mnaona nimeshafika hapa''
Rais
wa Tanzania John Pombe Magufuli mara tu baada ya uzinduzi wa daraja la
Rusumo linalounganisha Tanzania na Rwanda ambalo amelizindua rasmi yeye
na mwenyeji wake Rais wa Rwanda Paul Kagame. ''Nimefurahi kwa sababu nimekuja kufungua daraja la Rusumo.
''Hii ni Historia kubwa inayojengeka kati ya Tanzania na Rwanda''. ''Lakini
nataka kuwahakikishia ndugu zangu wa Rwanda kuwa Tanzania itatoa
ushirikiano mkubwa sana kwa nchi ya Rwanda'' alisema rais Magufuli. Rais wa Rwanda Paul Kagame akihutubia hadhira hiyo alisema ''Tunataka amani,undugu urafiki na tunataka kufanya biashara ili kila mmoja wetu aweze kupata faida''
Ziara hii ya kwanza ya Rais Magufuli nje ya nchi yake inaangaliwa na
wengi hapa Rwanda kama ya kuanza ukurasa mpya wa uhusiano kati ya nchi
mbili. Miaka ya nyuma uhusiano huo uliingiwa baridi baada ya
Tanzania kuwatimua raia wa Kinyarwanda, kitendo kilichowakasirisha
viongozi wa Rwanda.
Hayo yalifwatia kipindi kigumu cha uelewano mdogo
baina ya nchi mbili kuhusu swala la mgogoro wa mashariki ya Congo. Rwanda
kama nchi isiyopakana na bahari kibiasha hutegemea sana bandari ya Dar
es Salam na hivi karibuni Rais Kagame alimsifu mgeni wake na kuahidi
kuiga mfano wake katika juhudi za kupambana na rushwa na ufisadi.
Rais
Magufuli kesho ataungana na wananchi wa Rwanda katika maadhimisho ya
miaka 22 ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari kabla ya kufanya mazungumzo
na wandishi wa habari akiwa pamoja na Rais Paul Kagame.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :