KOFFI OLOMIDE, FERRE GOLA NA FALLY IPUPA WAGUSWA NA KIFO CHA PAPA WEMBA
Posted in
Burudani
No comments
Sunday, April 24, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
SAA chache baada ya kuripotiwa kifo cha Nyota wa muziki wa Soukous ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- Papa Wemba, baadhi ya mastaa wa muziki huo nchini Congo na duniani akiwemo Koffi Olimide wamzungumzia.
Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo. Alikuwa maarufu katika micharazo ya muziki wa Soukous, Alikuwa mmoja kati ya wanamuziki maarufu sana barani Afrika na kote duniani.
Kauli ya Koffi Olomide
Asubuhi ya Jumapili April 24 2016 ndio zimeanza kusambaa taarifa za kifo cha mwimbaji Mkongwe kutoka Congo DRC aitwae Papa Wemba ambaye imeripotiwa amefariki baada ya kuanguka jukwaani akiwa anatumbuiza huko Ivory Coast.
Taarifa za kifo zimeendelea kuwafikia watu mbalimbali akiwemo mwimbaji mkongwe wa Congo DRC Koffi Olomide ambaye ameandika maneno machache kwenye ukurasa wake wa Instagram akisema ‘kwaheri Kaka, asante‘ na kuambatanisha picha yao ya pamoja ya siku nyingi kwenye hayo maneno.
Koffi Olomide amekua akitajwa kuwa mpiga gitaa wa zamani na mtunzi wa nyimbo kadhaa zilizoimbwa na Papa Wemba.
Fally Ipupa na Ferregola nao Wamzungumzia
Papa Wemba amefariki baada ya kuanguka jukwaani huko Abidjan Ivory Coast akiwa anatumbuiza kwenye tamasha ambalo lilikua linaonyeshwa LIVE kwenye TV, kutazama video ya tukio lenyewe tazama post zangu za nyuma.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :