WAKENYA WAGUNDUA MRADI WA BIASHARA YA UFUGAJI WA SENENE WATAMU WENYE VIRUTUBISHO

No comments
Saturday, April 23, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Na Bosire Boniface, Garissa
Wakati akiwa kwenye safari za kibiashara kuelekea magharibi mwa Kenya katika mji wa Kisumu mwezi Septemba, George Morara alisimama kwa ajili ya kupata kifungua kinywa huko Kopolos, akitazamana na mahali pa kula Ziwa Victoria.



Senene waliotiwa rangi ya dhahabu wamewekwa kwenye chokoleti katika duka la French chocolatier Sylvain Musquar huko Villers-les-Nancy, Ufaransa, tarehe 12 Oktoba, 2013. Ufugaji wa senene kwa ajili ya matumizi ya chakula cha binadamu yanaongezeka huko Kenya. [Jean-Christophe Verhaegen/AFP]

Wakati akimsubiri mhudumu wa hoteli kuchukua oda yake, Morara, mwenye umri wa miaka 37,alisema aligundua kwamba kulikuwa na wadudu aliwafikiria mwanzo kwenye supu ya mteja aliyekuwa jirani.
"Nilimtahadharisha kuhusu wadudu katika sahani yake," nilimwambia tena. "Kilichonishangaza mteja huyo aliudhika. Aliniambia hawakuwa wadudu bali senene, ambao aliwaagiza."

Kuangalia hapa na pale, Morara aligundua wanaume wengine wakila chakula chenye senene --biskuti za senene, soseji za senene na vyakula vingine vya kusaga. Licha ya mshangao wa ajabu, Morara, ambaye anasambaza ndizi kutoka eneo alilozaliwa la Kisii kwenda kwa wachuuzi mbalimbali katika soko la ndani la Kisumu, aliagiza mkate mdogo wa mviringo wenye senene. Mara ya kwanza aliutafuna kwa unagalifu sana lakini alifurahia ladha yake, aliiambia Sabahi.

Aligundua kwamba mkate ule ulikuwa mtamu sana ambapo aliamua kuagiza zaidi kwa ajili ya kula barabarani lakini pia kupanua biashara yake na kusambaza senene kwa wachuuzi wa ndani. "Nilikuwa Kisumu kuchukua oda kwa ajili ya kusambaza ndizi, lakini pia nilipata oda za kusambaza senene, ambazo nimekuwa nikizisambaza kutoka Oktoba," Morara alisema.

Mara aliporejea nyumbani huko Kisii, ambapo anamiliki shamba dogo, alianza kukamata senene, kwa kutumia taa ili kuwavutia, na kuwafuga. Kila senene wa kike hutaga mayai matano hadi kumi kwa siku. Kwa kipindi cha nusu mwezi, biashara ya Morara ilikuwa ya faida kubwa , ikizalisha kiwango cha faida kubwa kwenye uwekezaji kwa wiki.

"Kwa wiki, ninatumia shilingi 200 (dola 2.30) kulisha senene na ninazalisha kiasi cha shilingi 15,000 (dola 175)," alisema, akiongezea kwamba huuza kilogramu 50 za senene kila wiki. "Ninauza kilogramu moja ya senene waliochemshwa au kukaushwa juani kwa shilingi 300 (dola 3.50).”

Desturi ya kula wadudu ni ya kawaida miongoni mwa jamii za mashariki mwa Kenya. Kumbikumbi na panzi wanaonekana kama chakula kitamu miongoni mwa jamii za Kisii na Luhya, alisema Michael Teka, mwenye miaka 27, mkaazi wa Kakamega.

"Hadi hivi karibuni, mtu anaweza akakuta kumbikumbi katika soko la [chakula] na madukani. Siku zaidi za hivi karibuni senene pia wanapambana kupata nafasi katika maduka," aliiambia Sabahi. Ongezeko la mahitaji ya senene wanaoliwa limeleta tasnia ya kilimo inayofaa na chanzo mbadala cha lishe nchini Kenya, ambako usalama wa chakula ni tishio.

Kuna soko lisilitosheleza nchini Kenya na nje ya nchi kwa wadudu wanaoliwa, alisema Monica Ayieko, mchumi mlaji na profesa mshiriki katika Shule ya Usalama wa Chakula, Kilimo na Bioanuwai ya Chuo Kikuu cha Bondo.
Mwezi Mei, shule ilitoa mafunzo kwa kundi lake la kwanza la watu kuhusu jinsi ya kufuga senene bila ya gharama na kuwauza kwa matumizi ya ndani na kusafirisha nje, Ayieko alisema. "Kama ilivyo katika kila biashara mpya, kulikuwa na hali ya mashaka lakini sasa karibia wakulima 1,000 wa senene wanavuna faida za ufugaji," aliiambia Sabahi.

Faida za lishe za kula wadudu

Ayieko alisema kwamba miaka yake ya kufanya utafiti katika senene ilionyesha kwamba wadudu walikuwa na protini nyingi, chuma, shaba na zinki, na kuwala hakukuwa na madhara kwa binadamu. "Mikoa ya Nyanza na Magharibi mara nyingi inakabiliwa na kusumbuliwa na utapiamlo na pia inawekwa miongoni mwa mikoa yenye [kiwango] cha juu sana cha umasikini," Ayieko alisema. "Kimsingi biashara hii inaua ndege wawili kwa jiwe moja."

Kwa mujibu wa ripoti ya Juni 2013 iliyochapishwa na Shirika la Chakula na kilimo (FAO), ukamataji wa wadudu na kuwazalisha katika ngazi ya kaya au katika kiwango cha kiwanda unaweza kutoa fursa muhimu za kipato kwa watu katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea kwa kufanana.

Bado, kukubali kwa walaji ni miongoni mwa vikwazo vikubwa kuwafanya wadudu chanzo kinachopatikana cha protini, ilisema ripoti hiyo. "Wadudu kama chakula na mlo wameibuka kama suala muhimu mahususi katika karne ya ishirini na moja kutokana na kupanda kwa gharama za protini ya wanyama, chakula na usalama wa chakula, shinikizo la mazingira, ongezeko la watu na ongezeko la mahitaji ya protini miongoni mwa watu wa ngazi ya kati," FAO ilisema katika ripoti yake, iliyoitwa "Wadudu wanaoliwa: Matarajio ya baadaye kwa usalama wa chakula na mlo."

FAO ilipendekeza masuluhisho mbadala kwa desturi ya mifugo na malisho, na kusema ulaji wa wadudu unachangia vizuri katika mazingira, afya na utafutaji riziki wa watu. Kwa Robinson Njeru Githae, aliyekuwa msaidizi wa waziri wa sheria na mambo ya katiba, mwelekeo wa ufugaji wa wadudu kwa ajili ya matumizi ya binadamu unaendana na wito ulioleta ubishi ambao aliutoa miaka tisa iliyopita aliposhika nafasi hiyo.

Mwaka 2004, Githae alichochea mjadala mkali wakati alipowataka Wakenya kuongeza tabia yao ya ulaji kwa kula kumbikumbi, panya na mizizi kama njia ya kuondokana na utapiamlo. "Wakati huo nililiona kama suluhisho kwa njaa ya kudumu miongoni mwa Wakenya walio wengi," Githae aliiambia Sabahi. "Niliadhibiwa na kuitwa nisiye na hisia, lakini sasa nimetetewa. Wadudu sio chakula tu bali sasa pia ni biashara ya kiuchumi."
Chanzo: sabahionline.com

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .