Amina: Ubinadamu utazingatiwa wakati wa kufungwa kambi ya Daadab

No comments
Tuesday, May 31, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Zoezi la kufungwa kwa kambi ya wakimbizi ya Daadab ambayo imekuwa ni kambi ya wakimbizi takriban 3000 kutoka Somalia na kuwaregesha(kurudishwa) nchini kwao, litaendeshwa kiubinadamu. Hayo ni kwa mujibu wa Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Balozi Amina Mohamed.
Balozi Amina alitoa kauli hiyo katika mkutano wa ushirikiano wa wapatanishi watatu (Tripartite Agreement Partners),iliyohudhuriwa na Waziri wa mambo ya nje Serikali ya Somalia, Abisalam Omer na Mwakilishi wa Umoja wa mataifa (Representatives of the United Nations High Commissioner for Refugees in Kenya and Somalia). Watatu hao walikutana katika Ofisi ya Mambo ya Nje.
Mkutano huo uliangazia mapitio ya changamoto ambazo zimepelekea mafanikio duni ya zoezi la kuwarudisha nyumbani wakimbizi tangu kutiwa saini kwa makubaliano ya Novemba 2013. Balozi Amina alisema serikali ya Kenya ilikuwa tayari imeshaunda kikosi kazi ambacho kingeainisha utaratibu wa utekelezaji wa mpango huo kuhakikisha zoezi linaendeshwa kiubinadamu.
Kutokana na kushindwa kwa umma wa kimataifa kutekeleza ahadi zao kwa vitendo,mkutano huo ulionyesha hofu yao kuhusu kukwama kwa zoezi la kuwarudisha wakimbizi makwao ambayo inachangiwa na uzembe wa umma wa kimataifa.
Kwa upande wake Waziri Omer hakusita kutoa shukrani zake kwa taifa la Kenya kutokana na jinsi walivyojitolea kuwapa hifadhi Wakmbizi kutoka Somali kwa zaidi ya karne mbili sasa.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .