IAAF yawaongezea adhabu Kiplagat na wenzake

Posted in
No comments
Tuesday, May 31, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Rais wa Raidha Kenya (AK) aliyesimamisha, Isaiah Kiplagat
Shirikisho la riadha la Duniani (IAAF), imewaongezea adhabu maafisa watatu wakuu wa Shirikisho la Riadha nchini (AK), ambapo sasa watatumikia kifungo cha miezi sita zaidi ya kifungo cha awali, wakati ambapo Bodi ya maadaili ikiendelea na Uchunguzi dhidi yao.
Maafisa waliokutwa na rungu la IAAF ni pamoja na Rais wa AK, Isaiah Kiplagat, Makamu wake, David Okeyo na mwenyekiti wa kanda ya Mashariki, Joseph Kinyua ambao walifungiwa kujihusisha na mchezo wa riadha mnamo Novemba 30, mwaka huu kutokana na tuhuma za Ufisadi na tuhuma nyingine ambayo ni kukwamisha vita dhidi ya matumizi ya Pufyaa (madawa ya kusisimua misuli).
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa jopo lililoteuliwa kuwachunguza maafisa hao, Shara Rao, adhabu dhidi ya watatu hao imeongezwa na kwamba sababu zilizopelekea hatua hiyo kuchukuliwa ni kutokana na kutokuwa tayari kwa jopo hilo.
“Sababu kuu ya kuongeza kwa adhabu dhidi ya Kiplagat na wenzake ni kutokana na jopo letu kutokuwa tayari kuendelea na uchunguzi, kuna mambo ambayo yamejitokeza, hii haina uhusiano na juhudi za kupiga vita matumizi ya pufya, pia ieleweke kwamba swala hili linahusiana na maswala ya Qatar na Nike," alisema Rao na kuongeza.
“Tunasubiri kupata taarifa kutoka kwa Shirikisho la Riadha la Qatar. hawajatujibu mpaka sasa. pia tunaendelea na uchunguzi kuhusu malipo yaliyofanywa na kampuni ya Nike, ili kupata ukweli kuhusu malipo hayo, je ni kweli malipo hayo yaliingia katika mifuko ya watu binafsi au yalielekezwa kusiko?" alisema.
"Aidha kuna mashahidi muhimu ambao bado tunahitaji kuwahoji, mashahidi hawa hawakuweza kupatikana ndani ya muda ambao adhabu ya wahusika hawa ilitamatika (Machi 29), tulikuwa hatujamaliza kazi yetu," aliongeza. 
Mbali na watatu hao, Afisa mkuu mtendaji (CEO), Isaac Mwangi bado anatumikia adhabu yake ya awali ambayo inatamatika mwezi Agosti  na hii ni baada ya rufaa yake aliyoiwasilisha kwa Bodi kuhusu madai ya kuhusika katika upokeaji wa Hongo (rushwa), kwa lengo la kuwalinda wanariadha waliokutwa na hatia ya kutumia Pufya kukataliwa.
Chanzo: Citizen Tv

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .