Harnonize: 'Sijamvisha mtu Pete'
Posted in
Burudani
No comments
Saturday, May 21, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Msanii kutoka katika label WCB Wasafi Harmonize ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake mpya wa ‘Bado’ amefunguka kuhusu mahusiano yake.
Staa huyo amesema kuwa katika maisha yake ya hajawahi kuvalishwa pete ya uchumba na wala yeye hajawahi kumvalisha mtu pete ya uchumba na kudai mpenzi wake mpya Jackline Wolper amemkuta akiwa hana mtu na ndiyo maana wakaweza kuanzisha mahusiano.
Harmonize amesema hayo kupitia kipindi cha Enews ambapo alikuwa anaelezea mambo mbalimbali kuhusu maisha yake mapya katika mahusiano na Wolper ambaye yeye mwenyewe amekiri kuwa ni mtu aliyeanzisha naye mahusiano hivi karibuni na kusema tuwe na subira kila kitu kitakuja kuwekwa wazi siku za usoni.
“Unajua mpaka saizi sijamvisha mtu pete ya uchumba wala mimi sijawahi kuvishwa pete ya uchumba ila niseme tu ni kweli nipo kwenye mahusiano na Wolper ambaye ni maarufu kama mimi na wakati ukifika kila kitu kitawekwa wazi” alisema Harmonize
Habari Zingine
- Timbulo: SIjarejea kwenye ualimu
- Vijana wazidi kujitokeza usaili wa Maisha Plus East Africa, Dar es salaam yatia fora
- RAPPER WA CAMEROON, NGOMA AACHIA VIDEO YA WIMBO MPYA ‘ALL LES DAY’, AIELEZEA COLLABO YAKE NA RAY VANNY
- New Hit: Lady Jay Dee – Sawa Na Wao
- Madonna atembelea makazi duni ya Kibera, Nairobi
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :