Askari Magereza Migori-Kenya wamjeruhi Mwanafunzi kwa kumpiga Risasi

No comments
Friday, May 27, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Askari Magereza mjini Migori, nchini Kenya ambao walikuwa wanamkimbiza Mfungwa ambaye alitoroka gerezani, wamemjeruhi kwa kumpiga risasi mwanafunzi mmoja wa Sekondari.
Inadaiwa kuwa risasi hiyo, iliyofyatuliwa kutoka katika bunduki ya mmoja wa askari magereza hao, aina ya G3 assault rifle, ilimpiga Mwanafunzi wa kidato cha pili, shule ya sekondari ya Ulanda ambaye alikuwa akitazama mechi ya mpira wa mikono 'Handball' kwenye mashindano ya shule ya upili, kanda ya ziwa.
Taarifa hizo zinaendelea kueleza kuwa Mfungwa huyo ambaye alikuwa uchi, alikimbilia shuleni hapo huku Maaskari wa gereza wakimbiza kwa lengo la kumkamata na kumrudisha Gerezani.
Kwa mujibu wa madaktari katika Hospitali ya St Joseph Ombo Catholic, ambapo majeruhi huyo alikimbizwa kwa ajili ya matibabu, Risasi hiyo iliondolewa katika moja ya macho yake.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo waliliambia gazeti la kila siku la Kiingereza la Daily Nation kuwa, baada ya tukio hilo, taharuki ilitanda miongoni mwa wanafunzi wengine waliokuwa wakitazama mechi, baada ya kusikia milio ya bunduki zaidi ya 10.
Tukio hilo linaripotiwa kusababisha vurugu kubwa katika eneo hilo ambapo inadaiwa kuwa wananchi sasa wanashinikiza serikali kufunga gereza hilo na kuwachukulia hatua Askari gereza, kwani wamekuwa na kawaida ya kufurahia kufyatua risasi hovyo.
Maandamano ya wananchi wenye hasira kali lilielekea hadi katika ofisi za Polisi, Kaunti wa Migori na kufanya mazungumzo na Kamanda wa Polisi, David Kirui ambaye alisema wahusika (Askari Magereza) hao watakamatwa na kuchukuliwa hatua ambayo ni pamoja na kufikisha Kortini.
“Askari wa magereza wamekuwa wakituangusha sana, unaanzaje kupiga risasi ya moto wanafunzi walipo? tayari tumeshaanzisha uchunguzi kuhusu vitendo vya maaskari magereza wote wanaofanya katika gereza letu, nimefadhaishwa sana na tukio hili," alisema Kirui.
Tutaendelea kukupasha habari zaidi kuhusu tukio hili kadri zitakapotufikia. endelea kutembelea Sauti Kuu kwa habari za siasa, Biashara, michezo na burudani kutoka kila pembe la Dunia.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .