Besigye ashitakiwa kwa Uhaini
Posted in
afrika mashariki
No comments
Monday, May 16, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.
Alikamatwa baada ya kuandaa sherehe zake mwenyewe za kuapishwa kabla ya sherehe za kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni aliyechaguliwa kwa muhula wa tano.
Kiongozi huyo amekuwa kizuizini muda mwingi tangu February mwaka huu. Rais Museveni amekanusha madai ya kuiba kura.
Ulinzi ulikuwa umeimarishwa kwenye sherehe za kuapishwa kwa Museveni Alhamis iliyopita ikiwa pamoja na kuzuiliwa kwa maandamano ya upinzani. Serikali iliwaonya waandishi habari kutoripoti maandamano yoyote.
Mitandao ya kijamii kama vile Whatsapp, Facebook na Twitter Ilizuiliwa kwa agizo la serikali ikidai ni sababu za kiusalama.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :