Dr. Matiang'i akerwa vyuo vikuu vya umma nchini kutumika kama handaki la ukabila

No comments
Saturday, May 28, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Waziri wa Elimu, Dr. Fred Matiang’i amesema serikali haitoruhusu Vyuo vya elimu ya juu (University) kuendelea kugeuzwa handaki la Ukabila.
Akizungumza kwenye mahafali katika chuo kikuu cha Katoliki cha Afrika mashariki, Catholic University of Eastern Africa, Dr Matiang’i alisema Vyuo vikuu vingi vya humu nchini havina taswira ya U-kenya bali ni machimbo ya makabila na ukabila.
“Vyuo vikuu vya umma, vinaendeshwa kwa fedha za mlipa kodi, na hatuwezi kuviruhusu vigeuzwe mahandaki ya ukabila, lazima zisalie kuwa taasisi za taifa," alisema Matiang'i.
Waziri huyo ambaye utendaji wake na kasi yake inaendana na sera ya Rais wa Tanzania, John Magufuli ya 'hapa kazi tu' alisisitiza kuwa mameneja wa Vyuo vikuu lazima wasimamie vigezo vilivyowekwa kisheria katika uteuzi wa Maafisa wakuu wa idara (Faculty Officials).
“Watu waajiriwe kwa kuzingatia vigezo tulivyoviweka, lakini sio kuajiri kwa kuangalia ukabila na namna mnavyofahamiana," alisema
Aidha Waziri huyo alisema Serikali imejipanga kufanyia mapitio utaratibu wa uteuzi unaotumika katika vyuo vikuu vya Umma ambapo alisema ndiko ambapo matatizo sugu ya ukabila yaliko.
Wakati huo huo, Dr Matiang’i aliwataka wahusika wote katika Vyuo vya umma kufanyia kazi, utofauti mkubwa unaojitokeza kati ya mitaala ya masomo katika vyuoni na hali halisi na uhitaji wa sasa katika soko la ajira.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .