Alikiba: Siwezi kuishi kama wao
Posted in
Burudani
No comments
Saturday, May 28, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Licha ya kusaini mkataba mkubwa na kampuni ya muziki ya Sony Music, Staa wa Bongo fleva, Alikiba amesema yeye kamwe hawezi kubadilika na ataendelea kuishi maisha ya kawaida.
Kiba ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wa ‘Aje’ alisema yeye anaishi maisha ambayo amechagua yeye na kamwe hawezi kuishi maisha kama ambavyo wasanii wengine wanaishi kwa sababu anapenda kuishi maisha ya kawaida na si maisha ya kisupa staa.
"Unajua mimi haya maisha nayoishi nimechagua, sipendi kuishi maisha ya kistaa kama wengine hata sasa licha ya kupata dili hili, nitaendelea kuishi maisha yangu ya kawaida, ningetaka kuishi kisupa staa uwezo huo nilikuwa nao hata kabla ya dili hili," alisema Kiba
Aidha, Msanii ambaye amewahi kutesa na vibao kama vile, Cheketua, Mwana, Njiwa na nyingine kibao, alisema dili la Sony Music na mafanikio mengine aliyopata ndani ya muda mfupi toka amerudi kwenye gemu, anaona ni kama amepiga msamba na si hatua tu.
Habari Zingine
- Madonna atembelea makazi duni ya Kibera, Nairobi
- Timbulo: SIjarejea kwenye ualimu
- Vijana wazidi kujitokeza usaili wa Maisha Plus East Africa, Dar es salaam yatia fora
- RAPPER WA CAMEROON, NGOMA AACHIA VIDEO YA WIMBO MPYA ‘ALL LES DAY’, AIELEZEA COLLABO YAKE NA RAY VANNY
- New Hit: Lady Jay Dee – Sawa Na Wao
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :