Watoto wa Beckham wanapenda 'sketi' balaa

Posted in
No comments
Saturday, May 28, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Nyumbani kwa mwanasoka mstaafu David Beckham na mke wake Victoria Beckham, jijini Marekani hakukaliki Aisee! Victoria (41), kafunguka kwamba yeye na mumewe, hawana amani nyumbani kutokana na watoto wao watatu wa kiume kuwaumiza vichwa kwa tabia ya kupenda mademu kupita maelezo.

Victoria anayefahamika kama mama mkali sana asiyependa masihara sasa anajikuta katika wakati mgumu kuwadhibiti vijana wake hao wanaozidi kukua na hivyo kuzidi kuwa na tamaa za kimwili.

Mvulana wao mkubwa anayejulikana kwa jina la Brooklyn (17), ndiye anayesumbuliwa zaidi na joto la mapenzi ya ujana kiasi kwamba ameanza kuwaathiri wadogo zake Romeo (13) na Cruz (11), kwa mujibu wa maelezo wa rafiki wa karibu wa familia hiyo ya 'kishua'

"Victoria na David wameanza kuwa na wasiwasi hasa kuhusu Brooklyn ambaye kageuka sukari ya warembo. Hawafahamu kabisa yupi ni demu wa Brooklyn kwa sababu kila wiki wanamuona na demu mpya, Naye Romeo ameanza kuonesha dalili za kuzifuata nyayo za kaka yake.

Kuna demu anayefanya kazi katika kampuni ya uwanamitindo ya mama yake ambaye kamtoa uchizi Romeo. Naye Cruz yupo njiani kufuata nyayo za kaka zake, anapenda sana mashindano ya pikipiki lakini ameanza kuonesha kuvutiwa na mademu, "alisema rafiki huyo.

David na Victoria walianza uhusiano wa kimapenzi mwaka 1997 na kisha wakafunga ndoa mwaka 1999. Penzi lao linazidi kuimarika licha ya changamoto za hapa na pale.

Mwanaspoti kenya

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .