Dkt Bilal apokea maandamano ya maonyesho ya vikundi vya wakulima mjini Morogoro
Posted in
No comments
Saturday, July 27, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti, mmoja kati ya
wachangiaji bora wa kuendeleza Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania
(MVUWATA) Justice Shekilango, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya
Jumuiya hiyo iliyofanyika leo Julai 26, 2013 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro.
Wasanii wa kikundi cha ngoma ya Muhembe cha
mjini Dodoma, wakitoa burudani wakati wa sherehe hizo za maadhimisho ya miaka
20 ya Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) yaliyofanyika leo
katika Uwanja wa Jamhuri mijini Morogoro.
Wakulima wa Jumuiya ya Mtandao wa Wakulima wa
Tanzania (MVUWATA) wakiwasili kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwa
maandamano leo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo,
yaliyopokelewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, aliyekuwa mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wanamtandao wa Jumuiya ya wakulima wa Tanzania (MVUWATA) baada ya kupokea rasmi
maandamano ya wakulima ya maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika
leo katika uwanja wa Jamhuri mijini Morogoro. Picha na OMR.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :