KENYA: MATOKEO YA MITHANI YA KIDATO CHA NNE (KCSE) YATANGAZWA LEO
Posted in
afrika mashariki
No comments
Thursday, March 3, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Akitangaza matokeo hayo mapema leo, Waziri wa Elimu, Dkt. Fred Matiang'i, alisema kuwa kaunti zote kote nchini zilikumbwa na tatizo la udanganyifu katika vyumba vya mitihani isipokuwa kaunti ya Isiolo huku Kaunti ya Nairobi, Makueni na Meru zikiripotiwa kuongoza kwa wizi wa mitihani.
Aidha Dkt. Matiang'i aliema tofauti na ilivyo kawaida,mwaka huu serikali ya Kenya imeamua kutofuta matokeo ya shule zilizokutwa na kosa hilo bali imewatia matokeo wanafunzi waliohusika na kosa la udanganyifu na kuongeza kuwa wanafunzi wanafunzi kutizama matokeo yao kupiia simu za rununu, kwa kutuma ujumbe mfupi wenye namba zao za mitihani, kwenda 22252.
Kwa mujibu wa Dkt. Matiang'i, ripoti ya mwaka huu ina maelezo ya kina tofauti na ripotiya mwaka jana na miaka ya nyuma. Waziri huyo anatakutana na waandishi wa habari baadae jioni ya leo kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa kina kwa maswali ya wanahabari kuhusiana na maswala yaliyoibuka kutokana na kutangazwa kwa matokeo hayo.
IDADI YA WATAHINIWA
Jumla ya watahiniwa 525,802 walifanya mitihani ya Kidato cha nne, Kenya Certificate of Secondary Education (KCSE), idadi ambayo ni ongezeko la asilimia 8.3 kutoka 485,547 waliofanya mtihani mwaka jana.
ili kupata matokeo kwenye mtandao bonyeza: http://www.knec.ac.ke/
ili kupata matokeo kwenye mtandao bonyeza: http://www.knec.ac.ke/
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :