ARUSHA: MITUMBA KUPIGWA MARUFUKU AFRIKA MASHARIKI

No comments
Wednesday, March 2, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliokutana leo mjini Arusha, Tanzania wameamua kupiga marufuku uagizaji wa nguo za viatu kuu vya mitumba. Utekelezaji wake utakuwa baada ya miaka mitatu.

Marufuku hiyo ni moja ya hatua zilizopendekezwa ilikuinua viwanda vya nguo katika kanda ya Afrika Mashariki. Serikali za Afrika Mashariki zimekuwa zikilaumu uagizaji wa nguo na viatu vilivyotumika kama moja ya sababu zinazofanya viwanda vya nguo na ngozi kusambaratika na hivyo kuwanyima wenyeji nafasi ya ajira.
 
Nguo hizo hutegemewa sana na watu wenye mapato ya chini kutokana na bei yake nafuu. Kadhalika, wauzaji wa nguo hizo wasafirishaji,waagizaji wote huzitegemea kupata mkate wao wa kila siku hii ikichangia pato la nchi na ajira kwa maelfu ya watu ambao huhudumu katika biashara hiyo.


Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli wa Tanzania ambay ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, akihutubia  Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya hiyo, jijini Arusha leo Machi 2, 2016
Viongozi hao pia watajadili pendekezo la kupunguza kiasi cha magari yaliyotumika yanayoingizwa kanda hii. Lengo lao likiwa kutafuta mbinu ya kusaidia viwanda vya utengenezaji magari vinavyoendesha biashara Afrika Mashariki.

Marais Paul Kagame (Rwanda), Uhuru Kenyatta (Kenya) na Yoweri Museveni (Uganda) walihudhuria mkutano huo mjini Arusha.

Maombi ya Sudan Kusini na Somalia kutaka kujiunga na jumuiya hiyo pia yalijadiliwa.
Sudan Kusini ilikubaliwa kujiunga kama mwanachama wa 6 wa muungano wa mataifa ya Afrika Mashariki. Wakati wa mkutano huo, viongozi hao wanatarajiwa kuzindua pasipoti ya pamoja ya Afrika Mashariki ambayo itakuwa katika mfumo wa elektroniki.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .