By
danielmjema.blogspot.com
Rais wa Tanzania John Magufuli na
mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta wanaweka jiwe la msingi katika barabara
itakayounganisha mji wa Arusha nchini Tanzania na mji wa Voi nchini
Kenya. Barabara hiyo kutoka Arusha hadi Taveta inatarajiwa kurahisisha uchukuzi na kuimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili. Ina
umbali wa kilomita 234 na ni sehemu ya mradi mkubwa wa barabara
inayotoka Arusha na kupitia Holili na Taveta hadi Mwatate. Jiwe la
msingi limewekwa na marais hao wawili eneo la Tengeru, Arusha.
Matukio katika picha:
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimkaribisha Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara
ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la
Arusha. |
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimkaribisha Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara
ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la
Arusha. |
|
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akizungumza jambo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya uzinduzi rasmi wa
Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya
jiji la Arusha. | | |
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimkaribisha Rais wa Uganda Yoweri Museveni
kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3
uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
|
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
amesimama pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Uganda, Yoweri Meseveni na
Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein wakati Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
ukipigwa kabla ya uzinduzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3
uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha. |
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akihutubia mamia ya wananchi wa Arusha hawapo pichani kabla ya ya uzinduzi rasmi
wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo
ya jiji la Arusha. |
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais Uhuru Kenyatta, wakiwaongoza Marais wa Uganda, Makamu wa Rais wa Sudani Kusini
pamoja na Burundi kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mitambo
itakayotumika katika ujenzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3
uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha |
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimwagilia mti maji pamoja na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika (Nairobi) Gabriel Negata mara baada ya uzinduzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi
Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
|
|
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
pamoja na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya Nchi. (PICHA NA IKULU YA TANZANIA) |
0 MAOINI :