Ghasia yatanda Misri, watu 75 wauawa.
Posted in
No comments
Saturday, July 27, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Wapinzani na wafuasi wa Mursi wakipambana mitaani mjini Cairo |
Kiasi ya watu 75 wameuwawa katika mapigano makali nchini Misri katika
maandamano makubwa baina ya mahasimu wanaounga mkono jeshi na wanaopinga
kuangushwa kwa rais Mohamed Mursi,anayechunguzwa kwa mauaji.
Mapambano yanaendelea katika hali inayozidi kuongezeka ya mvutano na
waungaji mkono wa itikadi kali za Kiislamu wa Mursi. Mkuu wa sera wa
Umoja wa Ulaya Catherine Ashton amelaani ghasia na mauaji vilivyotokea,
na kuzitaka pande zote nchini Misri kusimamisha vurugu mara moja.
Umwagikaji wa damu umeongeza hali ya wasiwasi kulikumba taifa hilo la Kiarabu lenye wakaazi wengi, na huenda hali hiyo ikachochea kuchukuliwa hatua muhimu na jeshi dhidi ya chama cha Mursi cha Udugu wa Kiislamu wiki tatu baada ya kuondolewa kutoka madarakani.
Katika jiji hilo lenye wakaazi wengi, mamia kwa maelfu ya Wamisri waliitikia wito wa mkuu wa majeshi jenerali Abdel Fattah al-Sisi kuingia mitaani na kutoa mamlaka ya kupambana na ghasia zilizotokana na kumuondoa madarakani hapo Julai 3 rais wa kwanza nchini Misri kuchaguliwa katika uchaguzi huru.
Chama cha udugu wa Kiislamu kilifanya maandamano yao, wafuasi wakimiminika na kujaza eneo linalokaliwa hivi sasa na waandamanaji ambao wako katika eneo hilo kwa muda wa mwezi sasa kaskazini ya Cairo kabla ya ghasia kuripuka.
Mwandishi habari wa shirika la habari la Reuters amejionea mapambano makali ya silaha katika majira ya asubuhi ya Jumamosi kati ya majeshi ya usalama na waungaji mkono wa Mursi, ambao walivunja mawe katika eneo la wapita njia na kuwarushia polisi.
Wingu la mabomu ya kutoa machozi lilitanda hewani.
Likimnukuu afisa wa polisi ambaye hakuwa na silaha, shirika la habari la Misri, MENA limeripoti kuwa watu tisa wameuawa katika ghasia nchini humo na kiasi watu 200 wamejeruhiwa. Msemaji wa kambi inayomuunga mkono Mursi amesema kuwa waungaji mkono wanane wa chama cha Udugu wa Kiislamu wameuwawa katika mapambano karibu na eneo linalokaliwa na waandamanaji kaskazini mwa Cairo pekee, na mwingine mwingine amesema kuwa walenga shabaha waliojificha juu ya nyumba walifyatua risasi.
Idadi rasmi
Idadi rasmi ya waliofariki , wengi wao ni kutoka mji wa pili nchini Misri wa Alexandria katika pwani ya bahari ya Mediterranean , ambako mamia ya watu walipambana vikali, kwa risasi na watu waliojificha juu ya majumba wakirusha mawe kwa makundi ya watu chini.
Wengi wa wale waliouawa wamechomwa visu, mahospitali yamesema , na kiasi mtu mmoja alipigwa risasi kichwani.
Baada ya al-Sisi kuwatolea wito waandamanaji kujitokeza kwa wingi, taarifa za uchunguzi dhidi ya Mursi kuhusiana na kutoroka kwake jela mwaka 2011 zimeashiria ongezeko la dhahiri la jeshi la nchi hiyo kupambana na kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani na kundi hilo la itikadi za Kiislamu.
Shirika la habari la MENA limesema kuwa Mursi ambaye amekuwa akishikiliwa katika eneo ambalo halijulikani katika eneo la kijeshi tangu kuondolewa madarakani, ameamriwa kuwekwa kizuwizini kwa muda wa siku 15 akisubiri uchunguzi.
Wasi wasi nchi za magharibi
Kuna hali ya wasiwasi katika mataifa ya magharibi kuhusiana na hatua ya jeshi dhidi ya Mursi, ambayo imezusha ghasia za wiki kadha katika taifa hilo la Kiarabu lenye ushawishi mkubwa linalopakana na mshirika mkubwa wa Marekani Israel.
Umwagikaji wa damu umeongeza hali ya wasiwasi kulikumba taifa hilo la Kiarabu lenye wakaazi wengi, na huenda hali hiyo ikachochea kuchukuliwa hatua muhimu na jeshi dhidi ya chama cha Mursi cha Udugu wa Kiislamu wiki tatu baada ya kuondolewa kutoka madarakani.
Waunga mkono jeshi
Katika jiji hilo lenye wakaazi wengi, mamia kwa maelfu ya Wamisri waliitikia wito wa mkuu wa majeshi jenerali Abdel Fattah al-Sisi kuingia mitaani na kutoa mamlaka ya kupambana na ghasia zilizotokana na kumuondoa madarakani hapo Julai 3 rais wa kwanza nchini Misri kuchaguliwa katika uchaguzi huru.
Chama cha udugu wa Kiislamu kilifanya maandamano yao, wafuasi wakimiminika na kujaza eneo linalokaliwa hivi sasa na waandamanaji ambao wako katika eneo hilo kwa muda wa mwezi sasa kaskazini ya Cairo kabla ya ghasia kuripuka.
Mwandishi habari wa shirika la habari la Reuters amejionea mapambano makali ya silaha katika majira ya asubuhi ya Jumamosi kati ya majeshi ya usalama na waungaji mkono wa Mursi, ambao walivunja mawe katika eneo la wapita njia na kuwarushia polisi.
Wingu la mabomu ya kutoa machozi lilitanda hewani.
Likimnukuu afisa wa polisi ambaye hakuwa na silaha, shirika la habari la Misri, MENA limeripoti kuwa watu tisa wameuawa katika ghasia nchini humo na kiasi watu 200 wamejeruhiwa. Msemaji wa kambi inayomuunga mkono Mursi amesema kuwa waungaji mkono wanane wa chama cha Udugu wa Kiislamu wameuwawa katika mapambano karibu na eneo linalokaliwa na waandamanaji kaskazini mwa Cairo pekee, na mwingine mwingine amesema kuwa walenga shabaha waliojificha juu ya nyumba walifyatua risasi.
Idadi rasmi
Idadi rasmi ya waliofariki , wengi wao ni kutoka mji wa pili nchini Misri wa Alexandria katika pwani ya bahari ya Mediterranean , ambako mamia ya watu walipambana vikali, kwa risasi na watu waliojificha juu ya majumba wakirusha mawe kwa makundi ya watu chini.
Kiongozi aliyeondolewa madarakani Mohammed Mursi |
Baada ya al-Sisi kuwatolea wito waandamanaji kujitokeza kwa wingi, taarifa za uchunguzi dhidi ya Mursi kuhusiana na kutoroka kwake jela mwaka 2011 zimeashiria ongezeko la dhahiri la jeshi la nchi hiyo kupambana na kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani na kundi hilo la itikadi za Kiislamu.
Shirika la habari la MENA limesema kuwa Mursi ambaye amekuwa akishikiliwa katika eneo ambalo halijulikani katika eneo la kijeshi tangu kuondolewa madarakani, ameamriwa kuwekwa kizuwizini kwa muda wa siku 15 akisubiri uchunguzi.
Waziri wa mambo ya ndani aliyewekwa na jeshi , Mohammed Ibrahim, amesema
ukaliaji wa eneo la mjini Cairo kwa muda wa mwezi mmoja sasa na wafuasi
wa Mursi , utafikishwa mwisho hivi karibuni kwa njia za kisheria,
gazeti la serikali la Al-Ahram limesema katika tovuti yake.
Jenerali Abd al-Fattah as-Sisi |
Kuna hali ya wasiwasi katika mataifa ya magharibi kuhusiana na hatua ya jeshi dhidi ya Mursi, ambayo imezusha ghasia za wiki kadha katika taifa hilo la Kiarabu lenye ushawishi mkubwa linalopakana na mshirika mkubwa wa Marekani Israel.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :