TAIFA STARS KUUMANA NA THE CRANES LEO; UWANJA WA NAMBOOLE-KAMPALA
Posted in
No comments
Saturday, July 27, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
LEO,
huko Kampala, Wenyeji Uganda, ambao walishinda 1-0 katika Mechi ya
kwanza Jijini Dar es Salaam, wanarudiana na Tanzania kwenye Mechi ya
CHAN kweye Uwanja wa Mandela, Namboole, ambao hawajafungwa tangu Mwaka
2004.
Mshindi wa Mechi hii atatinga Fainali za
CHAN, Mashindano maalum ya CAF yanayoshirikisha Wachezaji wanaocheza
Ligi za ndani ya Nchi zao tu, zitakazochezwa huko Afrika Kusini kuanzia
Tarehe 10 Januari 2014.
Wakati Uganda, ambao waliifunga Tanzania
Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 46 la Denis Iguma katika Mechi ya kwanza
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Wiki mbili zilizopita, wanahitaji sare
tu, Tanzania ni lazima washinde Mechi hii.
Kwa kutambua hilo, Kocha wa Tanzania,
Kim Poulsen, hapo Jana huko Kampala alitamka: “Unapocheza mechi za aina
hii za nyumbani na ugenini, huku mwenyeji akiwa anaongoza mabao yana
maana kubwa katika mechi. Mabao yanabadili mchezo na pia wachezaji
kifikra. Hivyo tuko hapa kwa ajili ya kufunga, ni lazima tufunge ili
tuweze kuendelea na mashindano. Lakini ngome yetu nayo ni lazima iwe
makini ili kutoruhusu bao.”
Lakini Uganda, chini ya Kocha kutoka
Serbia, Milutin Sedrojevic, na Nahodha wao Hassan Wasswa Mawanda, ni
Timu hatari na wenyewe wameshaahidi kuidhibiti Taifa Stars.
Katika Mechi ya leo, Uganda itawakosa
Mastraika wao wawili waliocheza Dar es Salaam, Patrick Edema na Tonny
Odur, kwani Edema ameenda Portugal kwa majaribio na Odur ni majeruhi
lakini wataongezewa nguvu kwa kurudi Uwanjani Beki wao wa kushoto Habib
Kavuma alieikosa Mechi ya kwanza kwa kuwa na Kadi.
UGANDA CRANES (Mfumo 4-2-1-3):
Hamuza Muwonge, Nicolas Wadada - Savio Kabugo - Richard Kasagga – Habibu Kavuma, Hassan Wasswa-Dennis Iguma, Joseph Mpande Saidi Kyeyune–Frank Kalanda – Brian Majwega
TAIFA STARS: (Mfumo: 4-3-3):
Juma Kaseja, Erasto Nyoni - Aggrey Morris - Kevin Yondon- David Luhende, Frank Damayo-Athumani Iddi-Amri Kiemba, Mrisho Ngassa-John Bocco - Salum Abubaker
REFA: Abduol Kanoso Ohabee [Madagascar]
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :