MAELFU WAUWAWA MISRI
Posted in
No comments
Sunday, July 28, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Wafuasi wa rais wa Misri aliyeondolewa madarakani na jeshi,Mohamed Morsi wamesema zaidi ya watu laki moja na ishirini wameuwawa katika mapambano na vikosi vya ulinzi na usalama mjini Cairo.
Polisi waliingia katika mkusanyiko wa usiku wa wafuasi wa Morsi saa chache baada ya waziri wa mambo ya ndani kusema wafausi wa Morsi na chama chao cha Muslim Brotherhood waliokusanyika kwenye viunga vya msikitini wa Rabba Al Adawiya lazima waondoke.Mwandishi wa BBC anasema ni mapigano mabaya zaidi tangu jeshi limuondoe rais Morsi madarakani.
Wakati huo huo, Uingereza imekemea matumizi ya nguvu yanayopoteza maisha ya watu nchini Misri.
Waziri wa masuala ya kigeni William Hague amewataka wenye mamlaka kumaliza mapigano na vurugu hizo.
Amesema wale waliohusika na mauaji hayo ni lazima wawajibike na haki ya wanaoandamana kwa amani ni wajibu ilindwe.
Bwana Hague pia amelitaka jeshi kuwachilia huru viongozi wa Muslim Brotherhood waliowekwa kizuizini akiwemo rais Mohamed Morsi.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :