DORTMUND YAITANDIKA BAYERN 4-2 FAINALI YA GERMAN SUPER CUP
Posted in
No comments
Sunday, July 28, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
BORUSSIA DORTMUND Jana Usiku kwenye Uwanja wao wa Nyumbani Signal Iduna Park walimaliza ule utawala wa hivi karibuni wa Bayern Munich kwenye Soka la German baada ya kuibonda 4-2 na kutwaa German Super Cup.
MAGOLI:
BV Borussia Dortmund 4
-Marco Reus Dakika ya 6 -Daniel Van Buyten 56 [Kajifunga mwenyewe] -Ilkay Gundogan 57
-Marco Reus 86
Bayern Munich 2
-Arjen Robben Dakika ya 54 & 64
Marco Reus ndie aliefungua na kufunga kitabu cha Magoli ya Borussia Dortmund kwa kufunga Bao la kwanza na la mwisho.Arjen Robben alijitahidi kuiletea Bayern
ushindi kwa kwanza kusawazisha na kuifanya gemu iwe 1-1 na baadae
kupunguza Mabao kuwa 3-2 lakini hiyo haikusaidia kwani Dortmund
walichachamaa na kupiga Bao la 4 kumuonyesha Kocha mpya wa Bayern, Pep
Guardiola kuwa kwenye Bundesliga kazi ipo.
AJAX YAIFUNGA ALKMAAR, YATWAA SUPER CUP
HUKO Holland, Siem de Jong alifunga Bao
la ushindi katika Dakika za Nyongeza 30 na kuipa Ajax Amsterdam ushindi
wa Bao 3-2 dhidi ya AZ Alkmaar baada ya kutoka nyuma Bao 2-0 na kutwaa
Holland Super Cup, rasmi kama Johan Cruijff Schaal, katika Mechi
iliyochezwa Jijini Amsterdam hapo Jana.
Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 0-0 na
Kipindi cha Pili AZ walipiga Bao mbili kupitia Johann Berg Gudmundsson
katika Dakika za 51 na 67.
Ajax walisawazisha katika Dakika za 69 na 75 kwa Bao za Christian Eriksen na Kolbeinn Sigthorsson.
Bao la ushindi la Ajax, lililofungwa na Siem de Jong, lilipatikana katika Dakika ya 103.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :