BARCELONA YAUA 7-0; MADRID IKICHOMOKA NA USHINDI WA 1-0
Posted in
No comments
Sunday, July 28, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
VIGOGO wa Spain, Barcelona na Real Madrid, waliendeleza maandalizi yao kwa Msimu mpya kwa kucheza Mechi za Kirafiki ugenini na Barca kuifumua Valerenga ya Norway Bao 7-0 na Real kuitungua Paris Saint-Germain Bao 1-0.
Majuzi Barcelona walipigwa Bao 2-0 na
Bayern Munich lakini Jana walikuwa mbogo na kuchapa Bao 7 huku
wakiongoza Bao 4-0 hapi Mapumziko.
MAGOLI YA BARCA:
-Alexis Sanchez Dakika ya 4-Cristian Tello 6-Lionel Messi 13
-Jonathan Dos Santos 42-Dongou 51 & 55 -Roman 87
Mechi zinazofuata za Kirafiki za
Barcelona ni Ziara yao huko Bara la Asia ambako Tarehe 7 Agosti
watacheza Nchini Thailand na Agosti 10 watakuwa Malaysia.
MADRID WACHOMOKA NA USHINDI WA 1-0
Nao Real Madrid Jana walipata ushindi wa
Bao 1-0 walipoifunga Paris Saint-Germain huko Sweden Mjini Goteborg
kwenye Uwanja wa Ullevi.
Bao la ushindi la Real lilifungwa katika Dakika ya 23 na Karim Benzema.
Mechi nyingine ya Real ni hapo Agosti 10 watakapocheza na Inter Milan.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :