HISTORIA YA MWANZILISHI WA TANZANIA-MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE.
Posted in
afrika mashariki
,
Kumbukumbu ya J.K. Nyerere
No comments
Monday, May 9, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha
Butiama wilaya ya Musoma vijijini mkoa wa Mara Tanzania (wakati ule:
TanganyikaAlikuwa mmojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa
kabila la Wazanaki Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya baba
yake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule
akitembea kilomita 30 hadi Musoma Baada ya kumaliza shule ya msingi
aliendelea kusomea shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora Katika
umri wa miaka 20 alibatizwa akawa Mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa
maisha yake. Mapadri wakiona akili yake kubwa walimsaidia kusomea
ualimu huko Makerere, Kampala Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945
Akiwa Makerere alianzisha tawi la Umoja wa Wanafunzi
Watanganyika, pia alijihusisha na tawi la
Tanganyika African Association (TAA).Baada ya kumaliza masomo ya ualimu
alirudi Tabora akifundisha shule ya
St.Mary.
Mwaka 1949 alipata 'Scholarship' ya kwenda kusoma kwenye Chuo
Kikuu cha Edinburgh , Uskoti Ufalme wa Muungano , akapata M.A. ya
historia na uchumi (alikuwa Mtanganyika wa kwanza kusoma katika chuo
kikuu cha Uingereza na wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya
Tanganyika). Aliporejea kutoka masomoni, alifundisha Historia,
Kiingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na
Dar es Salaam.
SIASA
Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika
African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa
mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere. Mwaka 1954 alibadilisha
jina la chama cha TAA kwenda chama cha Tanganyika African National Union
(TANU), ambacho pia kilikuwa
cha kisiasa zaidi kuliko TAA.
Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kikawa
tayari chama cha siasa kinachoongoza nchini Tanganyika. Uwezo wa
Nyerere uliwashtua viongozi wa kikoloni akalazimika kuchagua kati ya
siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akijisemea kuwa mwalimu kwa
kuchagua na mwanasiasa kwa bahati
mbaya.
Alijiuzulu ualimu na kuzunguka nchi nzima ya Tanganyika kuzungumza
na watu wa kawaida na machifu ili kuleta umoja katika kupigania uhuru
Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship Council na Fourth
Committee ya Umoja wa Mataifa Uwezo wake wa kuongea na wa kuunganisha
watu ulimwezesha kufanikisha
Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu Ushirikiano mzuri
aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati
huo, Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.
Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa
kuwa waziri mkuu mwaka 1960
WAZIRI WA TANGANYIKA HURU
Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9 Desemba
1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa
Tanganyika huru; mwaka mmoja baadaye akawa rais wa kwanza wa Jamhuri
ya Tanganyika.
Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika muungano wa
Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania mara baada ya mapinduzi ya
Zanzibar mwaka
1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.
Tarehe 5 Februari 1977 aliongoza chama cha TANU kuungana na chama
tawala cha Zanzibar Afro Shirazi Party na kuanzisha chama kipya cha CCM
(Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake wa kwanza.
Nyerere
aliendelea kuongoza taifa hadi 1985 alipomwachia nafasi rais wa pili,
Ali Hassan Mwinyi Aliacha kuongoza Tanzania ikiwa ni mojawapo kati ya
nchi maskini zaidi
duniani, ingawa yenye huduma za elimu na afya zilizoenea kwa wananchi
wengi.
Hata hivyo aliendelea kuongoza CCM hadi mwaka 1990 na kuwa na
athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake. Kwa mfano,
inasadikika kuwa Nyerere alishawishi uteuzi wa Benjamin W.Mkapa kama
mgombea wa urais mwaka 1995 ambaye alichaguliwa kuwa rais kwenye
uchaguzi
MAISHA BAADA YA KUSTAAFU UONGOZI
Nyerere alikaa muda mwingi kwake Butiama akilima shamba lake. Pamoja na
haya alianzisha taasisi yenye jina lake; mwaka 1996 alionekana akiwa
mpatanishi wa pande mbalimbali za vita vya wenyewe kwa wenyewe huko
Burundi
KIFO
Tarehe 14 Oktoba 1999 aliaga dunia katika hospitali ya St Thomas mjini
London Uingereza baada ya kupambana na kansa ya damu
MAFANIKIO
Kati ya mafanikio makubwa ya Nyerere kuna: kujenga umoja wa taifa kati ya watu wa makabila na dini tofauti, na hivyo kudumisha amani ya muda mrefu tofauti na hali ya nchi jirani, iliyofanya Tanzania iitwe "kisiwa cha amani".
Pia kustawisha utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili , kushinda ubaguzi wa rangi , kutetea usalama wa taifa katika vita dhidi ya mvamizi Idi Amin wa Uganda. Kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za Kusini mwa Afrika kama vile: Zimbabwe, Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO ), Angola (MPLA ) na Msumbiji (Frelimo).
KASORO
Nyerere analaumiwa kwa siasa yake ya kiujamaa kuwa ilichelewesha maendeleo ya kiuchumi wa Tanzania. Siasa yake ya ujamaa ilishindikana kwa kiasi kikubwa baada ya mwaka 1976 kwa sababu mbalimbali za nje na za ndani ya nchi. Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa ya kijamaa na kuwa hataweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa nyingine ambazo yeye hakuwa na imani nazo, Nyerere kwa hiari yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais kuanzia uchaguzi wa mwaka 1985 na kumwachia usukani Ali Hassan Mwinyi, aliyetawala kwa siasa ya uchumi wa soko huria.
Katika hali ya kukubali ukweli , Nyerere katika tafrija ya kumwaga alitamka juu ya siasa yake upande wa uchumi: “Nimefeli. Tukubali hivyo.”Kosa lingine ambalo wengine wanaona Nyerere alilifanya ni kumhadaa aliyekuwa Rais wa Zanzibar Mzee Abeid Amaan Karume kwa kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar, na kuanza kupora mamlaka ya Zanzibar kidogokidogo.
Kwa hivi sasa Wanzanzibari wengi wamechoka na Muungano huo, na wanataka uhuru wa nchi yao ili wapumue. Hata upande wa bara wananchi wengi wanalalamikia kutoweka kwa Tanganyika na serikali yake. Pia kuna makundi ya Waislamu wanaomtuhumu kwa kuendesha kwa siri vita dhidi ya dini yao na kupendelea Wakristo katika utoaji wa elimu na madaraka,japo wasomi wengi kwa kipindi cha utawala wake walikuwa Wakristo.
SIFA
Pamoja na hayo, Nyerere bado anakumbukwa na Watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake za kujali utu . Pia ataendelea kukumbukwa na Waafrika barani kote hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika.
Ni mmoja wa viongozi wachache waadilifu waliokwepa kujilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24.Mwishoni mwa maisha yake Nyerere aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama. Alipatwa na kansa ya damu akafariki Uingereza wakati wa kutibiwa katika mji wa London tarehe 14 Oktoba 1999. Alizikwa mahali pa kuzaliwa kwake, kijiji cha Butiama.

Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :