Muigizaji huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya kuzalisha filamu ya ‘RJ Company’, pamoja na Vicent Kigosi 'Ray', amekiambia kituo kimoja cha Redio nchini Tanzania kuwa, nje ya filamu yeye ni mjasiriamali wa biashara ya chakula.
“Mimi kama mimi ni mjasiriamali, kwa sasa nafanya biashara ndogo ndogo za maswala ya chakula yaani kupika. Kwa hiyo kama mtu akiwa na ofisi yake alafu anataka huduma yangu ya chakula, naandaa alafu nampelekea,” alisema Johari.
Johari amesema kazi hiyo amekuwa akiifanya kwa muda mrefu na inampatia kipato kizuri kwa kuwa ni miongoni mwa kazi ambazo anazipenda pia.

No comments:
Post a Comment